Pages

MUHAMBA

MUHAMBA
MUHAMBA HERBAL PRODUCTS

A.J.T.C

A.J.T.C
ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE

Monday, 24 November 2014

TAZAMA PICHA ZA MAZINGIRA YA NJE YA SHULE YA LUCKY VICENT ILIYOKO KWA MOROMBO ARUSHA

Huu ndio mwonekano halisi wa nje wa Jengo la Shule ya LUCKY VICENT kwa mbali

Jengo la shule ya LUCK VICENT Kwa karibu
Picha na; SAIDY LAZIMA

PICHA; Hali ya Uchafu katika soko la Morombo Jijini Arusha

Wafanyabiashara katika soko la kwamrombo wakiuza bidhaa zao pembezoni mwa Maji machafu
.
                                                          Picha na; KEPHAS DANIEL




Hali ya Uchafu katika soko la kwamrombo
                                                             Picha na; KEPHAS DANIEL


Mama JOHN maarufu kwa Jina la mama mbogamboga akichambua Mboga katika eneo lake la kufanyia biashara sokoni hapo
                                                             Picha na; KEPHAS DANIEL

Monday, 17 November 2014

Ajikata uume akitaka kuwa mwanamke

HABARI NA JASMIN R MUMWI 

              ataka kuwa mwanamke
Msanii Mrusi aliyecheza katika filamu mashuhuri ya 'Burnt by the Sun 2', alipoteza uume wake baada ya kujikata akitaka kuwa mwanamke.
Kikubwa kilichomfanya msanii huyo Evgniv Sapaev kujitaka sehemu zake za siri ni kwamba alitaka sana kuwa mwanamke.
Mwanamume huyo alionekana akotoka nje ya nyiumba yake huku damu ikimwagika kutoka kwa sehemu zak nyeti kufuatia upasuaji aliojifanyia mwenyewe.
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 38 ambaye nyota yake ilikuwa inang'ara sana alikimbizwa hospitalini kwa huduma ya dharura kwa hofu ya hali yake kuwa mbaya .
Madaktari walijaribu kumshona lakini hawakufanikiwa katika juhudi zao za kumrejeshea mwanamume huyo uume wake.
Afisaa mmoja hospitalini ambako muigizaji huyo alipokea matibabu alisema alikuwa na bahati sana kuponea kwani alivuja damu nyingi na kwamba angepoteza muda kidogo tu angefariki.
Kwa mujibu wa jarida la Mirror, jirani ya Evgniv Sapaev, Arkhip Tikhonov mwenye umri wa miaka 57 alishtuka sana alipombishia mlango na kujionea hali yake akiwa tayari ameanza kudhoofika kwani alikuwa amepoteza damu nyingi sana.
''Alionekana akitisha sana akiwa na damu mikononi mwake huku akishika sehemu yake ya uuma ambayo alikuwa ameikata. Nilidhani alikuwa anafanya mazoezi ya uigizaji, lakini alipozirai mlangoni huku akiwa ameshika sehemu yake ya siri mkooni ndipo nilipogudnua kuwa mambo yalikuwa mbaya,'' alisema jirani wa Evgniv.
Baada yua kupata nafuu mwathiriwa alinukuliwa akisema, ''tangu niwe mtoto mdogo nimekuwa nikijihisi kuwa mwanamke. Nilijaribu mara nne kukata nyeti zangu lakini wakati wote sikuwa na ujasiri wa kufanya hivyo.Lakini wakati huu niliweza kufanya hivyo baada ya kumeza tembe za kuzuia maumivu, na kujitaka kwa kutumia kisu.
Badhi walimkosoa msanii huyo kuwa kujikata sehemu zake za isiri badala ya kwenda hospitalini kwa upasuaji.chanzo bbc

Wito kwa wakazi kujihami dhidi ya Boko:H

OMBENI PELE.  Emir Sanusi alikuwa gavana wa benki kuu ya Nigeria kabla ya kuteuliwa kama Emir Kaskazini mwa Nigeriamir wa Kaskazini mwa Nigeria, ambaye ni mmoja wa viongozi wa kiisilmau wenye ushawishi mkubwa, ametoa wito kwa watu nchini humo kuchukua silaha na kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa kiisilamu wa Boko Haram.Emir huyo wa Kano, Muhammad Sanusi, amewaambia wakazi wasisubiri wanajeshi kuwalinda kutokana na magaidi.
Emir huyo ambaye alikuwa gavana wa benki kuu nchini humo kabla ya kuchukua wadhifa wake wa Emir, alitoa matamshi yake ya kutatanisha kwenye mkutano wa maombi.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kauli kama hii sio kawaida kutolewa kwani Emir huyo huyo hazungumzii sana maswala ya kisiasa.
Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwahangaisha wananchi kwa miaka mitano sasa
Wapiganaji wa wa Boko Haram wanaendelea kufanya mashambulizi ya mara kwa mara katika sehemu kadhaa za Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, huku wakiteka miji na mijiji ambko wamekuwa wakiwataka wakazi kufuata sheria kali ya kiisilamu.
Sanusi alikuwa mkosoaji mkuu wa serikali alipokuwa anafanya kazi yake ya benki, alisema kuwa watu hawapaswi kuogopa wanamgambo hao na kwamba wanapaswa kufanya wawezalo kujikinda kutokana na mashambulizi ya kundi hilo.
Mwandishi wa BBC anasema ingawa Emir huyo hakutaka kundi la Boko Haram, ilikuwa hatua ya kipekee kwa kiongozi kama huyo kuwataka watu kujihami dhidi ya Boko Haram.
Aanasema hii ni dalili tu ya mambo yalivyo nchini humo hasa katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.Chanzo BBC

Makamu wa rais Mugabe akana njama ya mauaji

na Jasmini Mwumwi
Joyce Mujuru amesema amewaamuru mawakili wake kumrejeshea hadhi yake ya kisiasa baada ya kuhusishwa na madai hayo ya uhaini pamoja na ufisadi.
Jarida la Sunday Mail la nchini humo, limeripoti kuwa kuna njama ya kumkodi mamluki kumuua Mugabe ili Bi Mujuru achukue mamlaka.
Mwezi jana Bwana Mugabe alifikisha miaka 90 na kusema hana nia ya kuachia madaraka.
Ametawala Zimbabwe tangu nchi hio kujipatia uhuru mwaka 1980.
Rais Mugabe akiwa na mkewe Grace Mugabe
Rais Mugabe na Bi Mujuru walikuwa wandani wa karibui lakini kwa sasa wamehasimiana huku mjadala wa kumrithi Mugabe ukitokota katika chama tawala cha Zanu-PF kikijiandaa kwa kongamano lake la kitaifa mwezi ujao.
Mkewe Bwana Mugabe, Grace Mugabe amekuwa akiendesha kampeini dhidi ya Bi Mujuru akimtaka astaafu.
Amemtuhumu Bi Mujuru kwa kuwa mtu wa kishetani na mwenye kugawanya watu pamoja na kujipatia pesa kwa njia ya udanganiyifu, kutoka kwa makampuni.
Taarifa ya bi Mujuru akikana madai ya njama hiyo haikutarajiwa.
Ingawa hajaonyesha dalili za kuachia ngazi, anakabiliwa na shinikizo kali sana za kisiasa.
Jarida la Sunday mail liliripoti taarifa hizo za kushtua kwamba bi Mujuru na washirika wake wanapanga kumkodi mamluki ambaye atamuua Mugabe ili achukue mamlaka.
"ninakanusha madai hayo ya uhaini na ufisadi pamoja na kutumia vibaya mamlaka yangu, madai ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi yangu kwa mda mrefu sasa,'' alisema Mujuru.
Amewataka mawakili wake kuchukua hatua za haraka za kisheria dhidi ya waliotoa madai hayo na kumharibia sifa yake. chanzo cha habari BBC swahili

  picha ya pamoja ya wakufunzi  wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha,watatu kutoka   kushoto waliokaa ni makamu mkuu wa chuo Bw Elifuraha Samboto.PICHA NA OMBENI PELE



mauaji yaendelea dhidi ya msako jijini Mombasa, KENYA



Na Jasmine R Mumwi                                                                                                                                      chanzo; BBC Swahili
Waumini wa kiisilamu wakifanya maandamano kupinga unyanyasaji Mombasa
Polisi nchini Kenya wamefanya msako mkali dhidi ya misikiti inayotoa mafunzo ya itikadi kali za kidini mjini Mombasa pwani ya Kenya.
Mtu mmoja ameuawa kwenye msako huo ulioanzishwa Jumapili dhidi ya misikiti inayosemekana kutoa mafunzo ya kuunga mkono harakati za kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab nchini Somalia.
Misikiti ya kwanza kulengwa katika msako huo ni ile ya Masjid Musa na Sakina.
Mkuu wa polisi mjini Mombasa alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa walipata taarifa kwamba kundi hilo limekuwa likipanga kufanya mashambulizi na hiyo ndiyo sababu ya msako huo kuanzis
Watu 200 wamekamatwa ikiwemo washukiwa wakuu sita.
Polisi wanasema kuwa mtu mmoja aliuawa ingawa hawajatoa taarifa zaidi kuhusu kifo cha mtu huyo na kwamba uchunguzi utafanywa.
Viongozi kadhaa wa kidini wameuawa mjini Mombasa katika kinachodaiwa kuwa mauaji ya kiholela huku kukiwa na ushindani pamoja na uhasama kati ya makundi kinzani ya kiisilamu.
Makanisa pia yamekuwa yakilengwa kwa mashambulizi.

Michezo ya kufuzu fainali za Euro 2016


 Habari na; SAIDY LAZIMA



Nani kufuzu kushiriki michuano ya mwaka 2016?
Michezo kadhaa imepigwa kuwania kufuzu fainali za Euro mwaka 2016


katika kundi A, Uholanzi imeichapa Latvia mabao 6-0,Jamuhuri ya Czech imetoka kifua mbele kwa mabao 2 dhidi ya 1 la Iceland, Uturuki nayo ikaiadhibu Kazakhstan kwa 3-1

Katika kundi B
Ubelgiji na Wales walitoka sare ya kutofungana, Cyprus imeitandika Andorra mabao matano bila majibu na Israel imeichapa Bos Herce mabao matatu kwa sifuri.

Kundi H lilikutanisha Azerbaijan na Norway ambapo,Norway iliondoka na ushindi wa goli moja kwa sifuri, Bulgaria ikatoka sare ya moja kwa moja na Malta, halikadhalika italia ilitoka sare ya moja kwa moja na Croatia.

Chanzao, BBC MICHEZO

Ahukumiwa kwenda jela kwa kumbaka mtoto.

Habari na; PROTTE MMANGA

Bukombe. Mtoto wa miaka (5) mkazi wa Kijiji cha
Kabuhima Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe
mkoani Geita amefanyiwa ukatili wa kinyama
baada ya kubakwa na jirani yao.

Mtuhumiwa anayedaiwa kufanya kitendo hicho
cha kikatili inadaiwa kuwa alimkuta mtoto huyo
anacheza mlangoni kwao akiwa hajavalishwa
nguo ya ndani na wazazi wake jambo lililpelekea
kufanya ukatili huo.

Akizungumuza na mwandishi wa habari hizi
mzazi wa mtoto huyo, Benja
mini Juma akiwa
kituo cha afya cha Uyovu akisubiri vipimo na
matibabu ya mtoto wake (jina tunalo) alimtaja
mtu anayedaiwa kufanya kitendo hicho kuwa ni
Juma Manjariwa anayekadiliwa kuwa na umri wa
miaka 28 ambaye wanaishi nyumba moja ya
kupanga

Alisema mwanae alikutwa na mkasa huo wakati
yeye akiwa ndani amepumzika baada ya chakula
cha mchana saa 7:37 mchana ambapo mama wa
mtoto alikuwa amekwenda kusuka kwa jirani.

Alisema aliamua kutoka nje na kukuta kijana huyo
anatoka nje na kuanza kukimbia, huku mtoto
akitokwa na damu nyingi sehemu zake za siri.

Mganga Mkuu wa kituo cha afya Kata ya Uyovu,
Joshua Mazingo alisema, “Mimi nikiwa safarini
nilipokea taarifa za mtoto hyuo ambaye
alifikishwa kwenye kituo cha afya kupimwa kisha
kukutwa na mbegu za kiume na kwamba
tunaendelea kumpima vipimo vingine kubaini
kama ameambukizwa magonjwa mengine ya
zinaa.” Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Geita,
Joseph Konyo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo
la kubakwa kwa mtoto na kwamba polisi tayari
wamemkamata mtuhumiwa na anatarajiwa
kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazomkabili.
Chanzo mwananchi.

DAR ES SALAAM:JAMII YATAKIWA KUTOWADHALILISHA WENYE ULEMAVU.

Habari na:MBONEA E. DANIEL.
Miriam Chirwa akiimba.


Mtaalamu wa malezi ya watoto wa shule ya Uhuru mchanganyiko Mwalimu Betha Kayolaameitaka jamii kuacha kutumia majina ya kuwadhalilisha  watu wenye ulemavu.
 
Akizungumza mara baada ya ibada katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Magomeni Mwembechai jana ambako kulikuwa na sabato maalum ya idara ya watoto, ambayo iliwaalika watoto wenye ulemavu kutoka shule ya uhuru mchanganyiko ya jijini Dar es salaam amesema kuwa, utumiaji wa majina yasiyofaa kwa watu wenye ulemavu ni kuwadhalilisha. 

Mbali na maneno hayo ya udhalilishaji mtaalamu huyo amesema kuwa vitendo  vya udhalilishaji vimekuwa vikiendelea ndani ya jamii ambapo baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wakiwaficha watoto wenye ulemavu na hata kuwafanyia vitendo vya ukatili hivyo akaomba makanisa ya Waadventista Wa Sabato kuwa karibu na kituo hicho katika kuwasaidia watoto wa shule ya uhuru Mchanganyiko. 

Jumla ya watoto 55 na walezi watatu  toka Shule ya Uhuru Mchanganyiko walihudhuria katika sabato hiyo ya wageni  ambayo iliongozwa na watoto wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Magomeni Mwembechai ambapo Mtoto mwenye ulemavu Miriam Chirwa aliimba.

Chanzo:Mtangazaji blog.



Picha za Lady Jay Dee video aliyofanya South Africa hizi hapa.

Habari na:Ombeni Pele:
Shabiki wa Lady Jay Dee kaa tayari kwa wimbo na video mpya kutoka kwa msanii wako, Mpaka sasa taarifa tulizopata wimbo unatoka tarehe 24 na video itatoka tarehe 28 mwezi huu. 

Video itazinduliwa M.O.G Bar & Restaurant.
 
 
 
 
 
 
 

Ebola yamfukuzisha kazi Waziri wa Afya wa Liberia


Habari na:Francis L. Matana:
Ebola yamfukuzisha kazi Waziri wa Afya wa Liberia

Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia amemfukuza kazi Walter Gwenigale Waziri wa Afya wa nchi hiyo na nafasi yake itachukuliwa na George Warner aliyekuwa mkuu wa zamani wa huduma za umma. 

Taarifa kutoka Monrovia zinasema kuwa, Walter Gwenigale amefutwa kazi kutokana na kushindwa kukabiliana na kasi ya homa ya ebola iliyotikisa nchini humo. 

Hata hiyo taarifa kutoka Ofisi ya Rais ya Liberia inaeleza kuwa, Gwenigale ataendelea kuwa mshauri wa Rais katika Kamati ya Ebola hadi atakapostaafu kwenye utumishi wa umma mwezi Februari mwakani.


Prof Maghembe asema urais si mashindano ya urembo

 Habari na; ELIETH MTAITA
Waziri wa Maji, Prof Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari

Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe ameshangazwa na utitiri wa watu wanaotaka kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2015, akisema nafasi hiyo ya juu nchini haifanani na mashindano ya urembo ambayo mtu yeyote anaweza kujaribu.

Mbunge huyo wa Mwanga alisema watu hao wanaojitokeza kuwania urais hawaelezi wanataka kulifanyia nini Taifa na akashauri wasioweza kueleza hoja zao wasichaguliwe kushika nafasi hiyo.

“Urais unahitaji kuwa na sifa, dira na ajenda kwa Taifa,” alisema Profesa Maghembe wakati wa mahojiano maalumu na gazeti hili mjini hapa.

Kauli ya Profesa Maghembe imekuja wakati Taifa likijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, 2015, huku chama chake, CCM kikikabiliwa na kazi ngumu ya kumpata mrithi wa Rais Jakaya Kikwete ambaye anamaliza muda wake.

Hali kama hiyo iliikumba CCM wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 wakati takriban watu 20 walipojitokeza kutaka kuingia Ikulu na baadaye mwaka 2005 wakati wa uchaguzi uliomuweka madarakani Rais Kikwete.

Ndani ya CCM, mjadala huo sasa umekumbwa na hoja ya umri baada ya makada vijana kujitokeza kutangaza nia ya kumrithi Rais Kikwete kupambana na wanasiasa wakongwe, baadhi wakiwa ni wale waliojiandaa kwa muda mrefu.

Hata hivyo, Profesa Maghembe alipuuza mjadala huo wa umri wa mtu kugombea urais akisema kuwa hauna msingi na kwamba sifa kuu ya mgombea urais ni ajenda ya kuliletea Taifa maendeleo endelevu.

“Umri hauwezi kuleta tofauti katika uongozi wa nchi. Ni kama kusema jiwe liwe rais,” alisema mwanasiasa huyo mkongwe, ambaye amefanya kazi wizara tofauti tangu Januari 2006 aliposhika uwaziri kwa mara ya kwanza.

Alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inataka mgombea urais awe na umri wa kuanzia miaka 40 na kuendelea.

“Hivyo haisemi kuwa ukishakuwa na miaka 70 huwezi kuwa rais ama haisemi ukiwa na miaka 40 unafaa zaidi kuwa rais. Inategemea huyo mtu anayegombea anataka kuwafanyia nini Watanzania,” alisema.

Waziri huyo wa saba tangu Wizara ya Maji ianzishwe, alisema kugombea urais kunategemea ajenda aliyonayo mtu na hata watu wanapokwenda kumchagua, lazima waangalie ana ajenda gani. “Ikulu si mahali pa kukimbilia, mimi hata sijui wanakimbilia nini kwa sababu lazima mtu uwe na ajenda. Na kama mnasikia mtu anasema mimi nataka kuwa tu rais, huyo hafai kabisa,” alisema.

“Lazima mtu anayetaka kuwa rais atueleze uchumi sasa unakua kwa asilimia saba na umekuwa hivi kwa karibu miaka 10 lakini ni jambo linalofanya umaskini uwe mkali kabisa na usiishe ni kutokana na shughuli inayofanywa na watu wengi ya kilimo, kuwapatia kipato haikui kama sekta nyingine.

Chanzo; MWANANCHI COMMUNICATIONS

Mujuru atuhumiwa kutaka kumuua Rais Mugabe

HABARI NA:Francis L. Matana
Mujuru atuhumiwa kutaka kumuua Rais Mugabe

Joice Mujuru Makamu wa Rais wa Zimbabwe anakabiliwa na tuhuma za kutaka kumuua Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo. Gazeti la Sunday Mail linalochapishwa Zimbabwe limeandika katika toleo la jana kwamba, Bi. Joice Mujuru pamoja na wasaidizi wake wawili wanahusishwa kwenye njama za kutaka kumuua Rais Mugabe aliyeiongoza nchi hiyo tokea ilipojipatia uhuru wake mwaka 1980.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, mirengo ya kisiasa ndani ya chama tawala cha ZANU PF inafanya juhudi ya kupata satua na ushawishi mkubwa kwa wanachama wa chama hicho, kabla ya kufanyika mkutano mkuu uliopangwa kuitishwa mwezi ujao. 
Bi Joice Mujuru amekuwa akishirikiana bega kwa bega na Rais Mugabe kwa kipindi kirefu, lakini katika miezi ya hivi karibuni amekuwa kwenye malumbano makali ya kisiasa na Grace Mugabe, mke wa Rais Robert Mugabe

 Grace Mugabe amekuwa akimtuhumu Joice Mujuru Makamu wa Rais kwa kupanga njama za kumpindua Rais Mugabe. Vita vya kugombania madaraka ndani ya chama tawala vimeshadidi baada ya Grace Mugabe ambaye ni mkuu wa umoja wa vijana wa chama tawala, kupata uungaji mkono mkubwa kutoka kwa Emmerson Mnangwaga mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama tawala cha ZANU PF

CHANZO: RADIO TEHRAN

Thursday, 13 November 2014

Uingereza yaandaa sheria kudhibiti IS


 Habari na; SAIDY LAZIMA



Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron
Uingereza inaandaa sheria kupambana na ugaidi, kuzuia ongezeko la Waingereza wanaokwenda kupigana nchini Syria na Iraq.


Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ameelezea kwa mara ya kwanza sheria hiyo inayopendekezwa yenye lengo la kuzuia ongezeko la Waingereza wenye itikadi kali wanaokwenda katika nchi hizo.

Waziri mkuu wa Uingereza ametangaza pendekezo la muswada huo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye bunge la Australia mjini Canberra.

Katika sheria hiyo, amesema polisi wamepewa uwezo mpya kuweza kukamata hati za kusafiria za wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wapya walioandikishwa na kundi la Islamic State, ambao wanajaribu kuondoka nchini humo.

''... Uwezo mpya waliopewa polisi katika bandari kukamata hati za kusafiria, kuwazuia washukiwa kusafiri na kuzuia raia wa Uingereza wanaorejea nchini humo isipokuwa tu wamefuata masharti yetu. Sheria mpya kuyazuia mashirika ya ndege ambayo hayata tii hatua zetu za kuwachunguza wasafiri, kuingia nchini Uingereza. Alisema Cameron.

Sheria hiyo inayopendekezwa pia itayatoza faini mashirika ya ndege ambayo hayatachukua hatua zaidi kuchunguza orodha ya abiria inayowabeba.
Serikali ya Uingereza inatarajia mswada huo utapitishwa kuwa sheria ifikapo mwishoni mwa Januari mwakani.

Chanzo; BBC

MAREKANI IMESEMA IMEFANIKIWA DHIDI YA IS


Habari na; MBONEA E. DANIEL                            
Mmoja ya wapiganaji wa Dola ya Kiislamu ( Islamic State)
Mkuu wa majeshi wa Marekani amesema kampeni ya miezi mitatu dhidi ya dola ya kiislamu Islamic State imekuwa na mafanikio, lakini akaonya Marekani na washirika wake walikabiliana na ugumu pamoja vikwazo kwa muda mrefu.

Naye Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Chuck Hagel akizungumza kwenye bunge la congress amesema dola ya kiislamu imedhibitiwa na hivyo haiwezi kusonga mbele na maeneo mengine imesambaratishwa japo wanaonekana kuendeleza ushawishi kwenye ukanda wa Iraq na Syria.

Mkuu wa kikosi cha majeshi ya Marekani Generali Jack Dempsey anakadiria idadi ya wanamgambo wa dola ya kiislam kufikia 31,000.

Marekani imekuwa ikifanya mashambulizi ya anga dhidi ya kundi hilo, ambapo pia limekuwa likitoa ushauri na mafunzo kwenye majeshi kwa majeshi ya Marekani.

Chanzo; BBC

Wednesday, 12 November 2014

UTAFITI WAONESHA VIJANA WENGI HAWATUMII KONDOMU KUJIKINGA NCHINI TANZANIA
Mwandishi: Edilitruda Chami 


Imeelezwa kuwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), yanaweza kuongezeka nchini hasa kwa vijana kutokana na kubainika kupungua kwa kasi ya matumizi ya mipira (kondomu).

Wataalamu wa Nishati na Madini watakiwa kuwa wabunifu.

 
NA FONIA BUNDALA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge amewasihi Watanzania kutumia teknolojia mpya  na za kisasa katika kuzalisha mazao na sekta nzima ya kilimo kwa ujumla ili kuzuia uharibifu wa mazingira ikiwemo misitu
.
Aliyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Ukuaji wa Uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi. Lililofanyika jijini Dar Es Salaam.
Alifungua Kongamano hilo kwa Niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Gharib Bilal.

Aliongeza kuwa Mikoa na Wilaya zote Tanzania  zinatakiwa kuweka sera endelevu ambazo zitaweza kuhakikisha kukabiliana na uharibifu wa Mazingira
.
Aidha alisema kuwa zipo juhudi ambazo Serikali imezichukua katika  kuhakikisha utunzaji wa  mazingira unatekelezwa na pia  kuzuia uharibifu wa mazingira kwa njia moja au nyingine.

Akiongea katika Kongamano hilo Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania Philippe Dongier alisema Kongamano hilo ni fursa adhimu kwa ajili ya majadiliano kuhusu program za maendeleo ya Tanzania zinavyoweza kustawi licha ya kuwepo kwa mabadiliko ya tabia Nchi. Hivyo basi Watanzania hawana budi kuwa waangalifu sababu mabadiliko ya Tabia Nchi yana athari kubwa.

SASA OBAMA MEZA MOJA NA PUTIN LICHA MVUTANO

NA FONIA BUNDALA

Rais Obama wa Marekani na Putin wa Urusi walikutana Jumanne mjini Beijing, kandoni mwa mkutano wa Jumuiya ya Ushirikisho wa Kiuchumi ya nchi za Asia na Pasifik - APEC . Kuzungumzia masuala ya Iran ,Syria na Ukraine.
 Rais wa Marekani Barack Obama na wa Urusi Vladimir Putin.
Uhusiano baina ya Marekani na Urusi uko katika kiwango cha chini kabisa tangu kumalizika enzi ya vita baridi, huku Urusi ikiekewa vikwazo vinavyoongozwa na Marekani kutokana na hatua yake ya kulitwaa eneo la Ukraine la Crimea mwaka huu, pamoja na mchango wake katika vita vya wale wanaotaka kujitenga mashariki mwa Ukraine

WANASHERIA MWANZA WAIFAGILIA WINDHOEK WASEMA NI BORA KWA AFYA

HABARI NA CHRISTINA KILOVELE









 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira akizungumza katika hafla fupi iliyowashirikisha baadhi ya wanasheria wa jiji la Mwanza kujadili bia za windhoek pamoja na maendeleo ya jiji hilo. Halfa hiyo ilikwenda sanjari na kila mgeni mualikwa kuchangia mada.
 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira (katikati), akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mmiliki wa  The Joint Pub iliyopo Isamilo jijini Mwanza.
 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira (kulia), akisisitiza jambo  katika hafla hiyo. Kulia ni Mmiliki wa  The Joint Pub, iliyopo Isamilo jijini Mwanza. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Hafla ikiendelea.
 Mdau wa Windhoek jijini humo naye alikuwepo 
kwenye hafla hiyo.
 Wanasheria wa jiji la Mwanza wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Mwanasheria Mtalemwa (wa pili kushoto), akiwa na wanasheria wenzake  wakifurahia Windhoek.
Kikao na hafla vikiendelea.

Dotto Mwaibale

BAADHI ya Wanasheria wa jiji la Mwanza wamesema unywaji wa bia ya Windhoek utasaidia kujenga afya za wanywaji kwani imetengenezwa kwa ubora wa juu ukilinganisha na bia zingine.

Wanasheria hao waliyabainisha hayo jijini Mwanza katika hafla fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Bia ya Mabibo kwa ajili ya kujua changamoto mbalimbali kutokana na soko la bia za Windhoek na Windhoek Draught na kupata maoni ya wadau wa vinywaji hivyo  iliyofanyika jijini humo mwishoni mwa wiki.

Mmoja wa wanasheria hao,   alisema kwa muda mrefu na familia yake amekuwa akitumia Windhoek na ajawahi kupata shida yoyote  kwani inachangamsha akili tofauti na bia zingine.

Bia hii haiwezi kumfanya mtumiaji ajisikie vibaya hata akinywa kiasi kikubwa na ndio maana mimi na wenzangu tunatumia bia hizi za windhoek.



"Iwapo tutajenga tabia ya kunywa bia hii hakika utafanya kazi zetu kwa uhakika hata tukiwa makazini kwani haitoi harufu mdomo na kulewesha ni vizuri  tukaiunga mkono Kampuni ya Mabibo Bia " alisema Mwanasheria huyo.

Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira aliwaomba wanamwanza kuiunga mkono Kampuni ya Mabibo Bia kwa kununua vinywaji vyake kwani mpango wa kampuni hiyo ni kujenga kiwanda ambapo kitakuza uchumi wa mkoa wa Mwanza na kutoa ajira kwa vijana.

VITA YA WAISLAM NA WAKRISTU GEITA YATISHIA WANANCHI, MCHUNGAJI ACHINJWA HADI KUUAWA, SHUHUDIA HAPA


Habari na, NEEMA MWAMPAMBA

Machafuko makubwa yametokea leo katika kijiji cha Buseresere Wilayani Chato Mkoani Geita kati ya waslam na wakristu na kupelekea watu 10 kujeruhiwa vibaya kwa mapanga huku mchungaji wa kanisa la Pentekoste Assemblies of God Mathayo Kachila (45) akipoteza maisha kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa ni waumini  wadini ya kiislam kisha mwili wake kutelekezwa kwenye vibanda vya maduka ambavyo vilikuwa jirani na eneo hilo.

Habari za kaminika eneo la tukio hilo lililotokea majira ya asubuhi zimeeleza kuwa chanzo cha machafuko hayo ni watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wadini ya kiislam kuvamia bucha lililokuwa likiwauzia nyama wakristo wa kijiji hicho waliokuwa wamepanga foleni kwa wingi kusubili huduma hiyo.


Imeelezwa kuwa Wakristu hao walikuwa wamechinjia ng'ombe mmoja na mbuzi wawili eneo la Kanisani kabla ya kuleta nyama hiyo katika bucha hilo lililopo eneo la Buselesele Sokoni na ndipo walipokumbana na kadhia hiyo ya waislamu.

Tukio hilo lilianza majira ya saa 2 asubuhi muda mfupi baada ya nyama kuwasili katika bucha hilo la wakristu kwa ajili ya kuuzwa jambo linalodaiwa liliwakera waislam ambao waliivamia bucha hiyo kwa lengo la kuifunga.


Wakati wakristo wakitafakari uwepo wa waislam kwenye bucha lao lililpambwa kwa maandishi BWANA YESU ASIFIWE,YESU NI BWANA, ndipo waislam ambao kwa wakati huo walikuwa wametapakaa mtaani kwa lengo la kuhamasishana waliongezeka eneo lilipo bucha hilo na kisha kuimwagia nyama iliyokuwa kwenye bucha hilo vitu vinavyodaiwa kuwa ni sumu.


Kutokana na hali hiyo wakiristo walionekana kukerwa na kitendo cha waislam kuimwagia nyama hiyo vitu hivyo na kisha mapambano yalianza baina ya wakristu na waislam ambapo mbali na wakristu kutumia mawe waislamu wao walitumia mapanga na majambia.


Hata hivyo wakati mapambano hayo yakiendelea mchungaji huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alifika eneo la tukio ili kujua kulikoni na ndipo naye alipojikuta akishambuliwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za kichwa chake na alifia njiani wakati akikimbizwa katika hospital ya Wilaya ya Geita kwa matibabu zaidi.


Mbali na mchungaji huyo kupoteza maisha,wengine waliojeruhiwa ni pamoja na Said Ntahompagaze(45),Sadick Yahaya(40),Yasin Rajab(56),Vicent Damon(22),wote wakazi wa Buselesele na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Ramadhani ambaye yuko mahututi katika wodi namba nane katika hospital ya wilaya ya Geita.


Hata hivyo watu wengine watano ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja walitibiwa na kuruhusiwa kutokana na hali zao kuwa nzuri.


Jeshi la polisi Wilayani Chato na Geita lilifika eneo la tukio hilo majira ya saa 4:30 na kukuta uharibifu mkubwa umekwishafanyika ikiwa ni pamoja na kukuta duka la Mwenyekiti wa BAKWATA wilaya ya Chato Yusuph Idd linalotumika kwa biashara ya M-Pesa na vinywaji baridi likiwa linateketea kwa moto uliodaiwa kuwashwa na waumini wa dini ya kiislam.


Mkuu wa Wilaya ya Chato Ludorick Mpogolo aliyefika eneo la tukio muda mfupi baada ya polisi kuwasili eneo hilo mbali na kusikitishwa na kitendo hicho aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiangalia njia sahihi za kutatua mgogoro huo ambao unakuwa kwa kasi kila kukicha.


Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula mbali na kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo, alionyesha kukerwa na watu ambao wanafurahia vurugu zisizo na msingi na kuonya kuwashughulikia wale wote watakaobainika ni wachochezi wa masuala ya kidini.

CHANZO; Geita yetu blog

AJTC

AJTC
ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLEGE