Pages

MUHAMBA

MUHAMBA
MUHAMBA HERBAL PRODUCTS

A.J.T.C

A.J.T.C
ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts

Wednesday, 3 December 2014

HABARI PICHA: MAHAFALI YA TISA YA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA (AJTC

Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) Bi NEEMA MWAIPELA akizungumza machache kabla ya mahafali ya tisa ya chuo hicho kuanza, yaliyofanyika katika ukumbi wa PPS Ijumaa mkoani Arusha.                                      ( Picha na Edilitruda Chami)


HABARI PICHA MAHAFALI YA TISA YA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA

katika picha ni baadhi ya wahitimu wa chuo cha uandishi  wa habari na utanganzaji  Arusha  wakiwa na mgeni rasmi alie kaa wapili kushoto pamoja na wakufunzi wao. picha na Christina Kilovele

HABARI PICHA:WAKUFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA.

Wakufunzi katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi kwenye mahafali ya tisa ya chuo hicho. (Picha na Glory Chacky)

HABARI PICHA

baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wakiwa kwenye mahafali ya tisa katika ukumbi wa PPS jijini Arusha. PICHA NA SINYATI KILUSU.

HABARI PICHA

wanafunzi wa darasa la AICC katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha bw. Sebastian Mnakaya(aliekaa)na bw.Bugoma wa Bugoma wakituma habari kwa njia ya mtandao mapema leo chuoni hapo.

PICHA NA JASMINE R MUMWI

HABARI PICHA: UWASILISHAJI WA SOMO KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA.

Wanafunzi wa chuo cha uandishi  habari na utangazaji Arusha wakifuatilia uwasilishaji wa somo katika ukumbi wa chuo hicho. (Picha na Emma Moshi)

Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. ONESMO ELIA MBISE akitoa hitimisho baada ya uwasilishwaji wa somo chuoni hapo hivi karibuni. (Picha na Mbonea E. Daniel)

Makamu mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. ELIFURAHA JOHN SAMBOTO akifurahia jambo wakati wa uwasilishwaji wa somo chuoni hapo. (Picha na Giftsilvano Msangi)

Mwanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na tangazaji Arusha, Mwanahawa Kitomari akifanya uwasilishaji wa somo chuoni hapo. (Picha na Veronica Mramboah)

HABARI PICHA MATUKIO

Mgeni rasmi katika mahafali ya tisa ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Fredrick Mumbuli ambaye amesimama katikati akihutubia katika mahafali hayo ambayo yalifanyika tarehe 28 mwezi wa 11 mwaka huu katika ukumbi wa PPS jijini Arusha. PICHA NA ESTHER A. CHAVALA

Tuesday, 2 December 2014

HABARI PICHA MATUKIO YA WIKI ARUSHA.

Wahitimu wa chuo cha uandishi wa habari na Utangazaji Arusha AJTC wakiwa katika mahafali ya tisa ya kuhitimu masomo yao ya ngazi ya stashada yaliyofanyika tarehe 28 mwezi 11 mwaka huu katika ukumbi wa PPS jijini Arusha. PICHA NA FONIA BUNDALA.

HABARI PICHA: MATUKIO YALIYOJIRI ARUSHA WIKI HII

Dokta Hamisi Kigwangala akilakiwa na waumini wa kanisa la KKKT Olorieni jijini Arusha Hivi karibuni

Dokta Kigwangalla akihojiwa na mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi Mussa Juma juu ya suala la Escrow account

Dokta Kigwangallah akitoa nasaha kwa wananakwaya wa kwaya ya Msifuni iliyozindua albamu yao ya Video hivi karibuni katika kanisa la KKKT Olorieni jijini Arusha hivi karibuni

Monday, 1 December 2014

MAKALA YA UCHUMI: UFUGAJI NYUKI UMEWAKOMBOA WASOMI KIUCHUMI






Wakiwa wanatengeneza mizinga ya kufugia nyuki mkoani Singida

Vijana wa kikundi cha Singida Youth Interprises and consultant cooperative society ambao ni wahitimu wa vyuo wanaojishughulisha na biashara ya ufagaji nyuki na uuzaji wa asali na nta


kijana Hamza Rajabu wa kikundi cha Singida Youth Interprises and consultant cooperative society ambao ni wahitimu wa vyuo wanaojishughulisha na biashara ya ufagaji nyuki na uuzaji akiwa kwenye maonyesho ya kongamano la ufugaji nyuki lililofanyika jijini Arusha hivi karibuni 


Na Ferdinand Shayo.Arusha.
Baada ya kuhitimu elimu ya chuo kikuu safari inaanza ya kuelekea kwenye jamii na kuanza maisha ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto zake ikiwemo suala la ajira ambalo ni suala mtambuka kwa kila mhitimu wa chuo.
Katika harakati za kufanya shughuli za kujiingizia kipato na kutengeneza ajira ,vijana 13 wa mkoa wa Singida ambao wote ni wahitimu kutoka vyuo mbali mbali wanakusanyika na kuanza kufuga nyuki pamoja na kuuza mazao ya nyuki ambayo ni asali,nta na sumu ya nyuki ambayo ni dawa.
Baada ya kuona fursa iliyopo katika sekta ya nyuki wanaamua kuitumia vyema kwa kuanza kufuaga nyuki na kuuza mazao yake ambayo yamewapatia faida za kiuchumi pamoja na kufanikiwa kuuza katika masoko ya nje.
Vijana hao walipohitimu chuo kikuu walijikusanya na kuunda kikundi cha Singida Youth Interprises and consultant cooperative society.
Mmoja wa wanachama wa kikundi hicho ni Hamza Rajabu anaeleza kuwa walianza kufuga nyuki wakiwa wenyewe baadae  wakaungana na vyama vya wafugaji nyuki ambapo tulivuna tani nyingi na kuiuza hadi soko la nje.
Hamza anaeleza kuwa changamoto kubwa iliyokua inawakabili ni ubora wa vifungashio (parking na lebel) lakini waliitatua kwa kupata mafunzo kutoka kwa wataalamu hivyo kufanikiwa.
Kama wahitimu tumefanikiwa kutengeneza vikundi 16 vya wafugaji nyuki na kuwapa ushauri wa kitaalamu,kutengeneza mabanda na vifaa bora vya kuchuja asali.
‘Binafsi nimehitimu chuo cha kilimo SUA mwaka juzi ,tunachokiona hapa kwenye sekta ya nyuki ni wajasiriamali wengi kukosa kuthibitishwa viwangoi na  TBS na  pia kupata vifungashio vizuri.  
Msimu uliopita tulizalisha tani 8 za asali na nta tani 18 kwa Mwekezaji kutoka Marekani .
Wahitimu wao ni kutoka vyuo mbali mbali ikiwemo  Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ,St.Agustine University (SUA).
Tunafanya biashara ya kuuza makundi ya nyuki katika sehemu mbali mbali ndani na nje ya Singida ,maeneo ya Nyumba ya nyuki na Iringa.
Wasomi hao wamefanikiwa kutengeneza makundi ya vijana,wazee na kinamama yanayojishughulisha na ufugaji nyuki.
Makundi hayo tunayapa mizinga miwili miwili kama mtaji ambao hutolewa na Mwekezaji kutoka nje kama mkopo wakivuna asali wanamuuzia mwekezaji huyo baada ya miaka miwili wanabaki na mizinga hiyo.
Mizinga inayotolewa ni ile ya kisasa ambayo huuzwa kiasi cha shilingi 65000 huwasaidia wafugaji kutunza asali nyingi ambayo wanaiuza na kuwapatia kipato.
Wakati mwingi tunatoa elimu kwa wafugaji nyuki namana ya kufanya ufugaji wa kisasa na kuvuna asali kwa kuzingatia usafi ,asali ambayo tunaiufungasha na kuiuza ndani na nje ya nchi.
Kwa sasa wanamiliki mashamba matatu ,moja kwa ajili ya kufuga makundi ya nyuki na kuyauza mengine ni kwa ajili ya asali,nta na sumu ya nyuki.
“Tuna mashamba matatu makubwa tunayatumia katika shughuli ya ufugaji kuku ,mawili yako Kisaki na moja liko wilaya ya Ikundi mkoani Singida.
Tunawashauri Watanzania na wasomi wenzetu wanaohitimu vyuo kutumia fursa lukuki zilizoko katika jamii zao na kujiajiri badala ya kusubiria kuajiriwa.
0765938008

Wednesday, 12 November 2014

MBOWE AICHAKAZA MIKOA YA KIGOMA NA KATAVI

  NA: GIFTSILVANO MSANGI


Akinamama wa kijiji cha Igalula mkoani Kigoma, wakicheza ngoma ya asili, wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (kushoto), baada ya kuwasili kijijini hapo, ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Wananchi wa kijiji cha Igalula mkoani Kigoma, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wakati alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwakabidhi kadi za Chadema waliokuwa viongozi wa CCM wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga katija jimbo la Mpanda Vijijini, baada ya kujiunga na Chadema katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Badhii ya waliokuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga katika jimbo la Mpanda Vijijini, wakimkabidhi kadi za CCM Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, walipoamua kujiunga na Chadema, baada ya mkutano wa Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kijijini Hapo juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisalimiana na Bi. Mariamu Ramadhani (86), baada ya kuwasili katika kijiji cha Kapalamsenga mkoani Katavi, ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Zanzibar), Salumu Mwalimu akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Waliokuwa viongozi wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga kupitia CCM, wakionyesha kadi zao kabla ya kuzikabidhi kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, walipojiunga na chama hicho wakati wa mkutano wa Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kijiji hapo juzi.

KIFO CHA PILI CHARIPOTIWA MALI KUTOKANA NA UGONJWA WA EBOLA

NA ESTHER A CHAVALA.
 
12 Novemba 2014


 tarangiremedia.blogsports.com

Muuguzi kutoka nchini Mali amekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola, kikiwa ni kifo cha pili tangu  Ugonjwa huo kudhibitishwa nchini humo.

FIKRA ZA OSAMA ZAFUNZWA KWA WATOTO PAKISTANI


NA EMMA MOSHI


  • 12 Novemba 2014

 tarangiremedia.blogsports.com


Kiongozi wa kidini nchini Pakistani Abdul Aziz Ghazi anayemiliki shule nane zinazofundisha msimamo wa Bin Laden anatoa mafunzo ya fikra za Osama bin Laden kwenye shule za dini kwa Wanafu

MREMA APOKELEWA KWA KISHINDO NA WANANCHI WA JIMBO LAKE

NA: GASPER MUSHI
Mkutano wa hadhara wa chama cha Tanzania Labour (TLP) uliokuwa ukihutubiwa na Mbunge wa jimbo la Vunjo Agustine Mrema jirani na matanki ya Maji katika kijiji cha Mieresini wilaya ya Moshi vijijini.
Afisa uhusiano wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Frolah Nguma (aliyesimama)akitoa ufafanuzi juu ya maswala ya maji baada ya Mbunge Mrema kumtaka kufanya hivyo muda mfupi baada ya maofisa wa Mamlaka hiyo kufika katika Matenki ya Maji kwa ajili ya ukaguzi wa kawaida.
Msimamizi mkuu wa (MUWSA) Kituo cha Himo Brucevictor Sangawe akitoa ufafanuzi kwa wananchi mbele ya mbunge wa jimbo la Vunjo ,Agustine Mrema juu ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo ya ukanda wa juu katika mji wa Himo.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Mbunge Mrema.
Mh Mrema akifuatilia maelezo ya maofisa wa Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) walipokuwa wakitoa maelezo kwa wananchi (hawapo pichani)  ,Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya kasakazini.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA UFUGAJI NYUKI ARUSHA

LOWASSA AZINDUA HELKOPTA YA GWAJIMA KWA KISHINDO



Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono waumini Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima,Kawe jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasili kwenye viwanja vya kawe lilipo Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima leo.

Wednesday, 22 October 2014

MTOTO ALIYETOROKA MOSHI AIBUKIA DSM









Mtoto Hassan Masasi, aliyetoroka nyumbani kwao Moshi, Kibosho-Umbwe, mkoani Kilimanjaro.

Mtoto Hassan Masasi (pichani), aliyetoroka nyumbani kwao Moshi, Kibosho-Umbwe, mkoani Kilimanjaro, ameonekana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana katika ofisi za gazeti hili zilizoko Mikocheni jijini Dar es Salaam, mtoto huyo mwenye umri wa miaka saba, alisema ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kindi Juu, iliyopo Moshi, Kibosho- Umbwe.

Alimtaja mama yake mzazi kuwa ni Pendo Athanas, mkazi wa eneo hilo na baba yake anaitwa asasi anayeishi Bukoba.
Hata hivyo, alisema wakati anaondoka nyumbani kwao, hakugombezwa na mtu yeyote wala kufanyiwa kitendo chochote kibaya isipokuwa aliamua mwenyewe kupanda basi la kampuni ya Buffalo bila kulipa nauli lakini alikuwa hajui anakokwenda.
Alisema alipofika Dar es Salaam, alipanda gari la kwanza akashuka na kisha kupanda lingine ambalo lilimfikisha eneo aliloliita ‘Bom-bom’ ambako alikuwa anatunzwa na msamaria mwema ambaye hamjui jina lake.

Mlinzi katika kampuni ya pikipiki iliyopo Mwenge mkabala na Kanisa la Efatha, jijini Dar es Salaam, Dotto Mkonda, alisema alimkuta mtoto huyo eneo la Mlalakuwa jana.

Dotto aliyemfikisha mtoto huyo katika ofisi za gazeti hili, alisema alimkuta katika kichochoro huku akiwa amechoka kiasi cha kuzungumza kwa taabu.

Alisema baada ya kumpa chakula, alimpeleka kituo kidogo cha polisi cha Mwenge ambako alifunguliwa jalada namba MWG/RB/1743/2014.

Amewataka watu wanayemfahamu mtoto huyo kwenda katika Kituo cha Polisi Mwenge ama cha karibĂș au kupiga simu namba 0716 87 86 41.

AJTC

AJTC
ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLEGE