Pages

MUHAMBA

MUHAMBA
MUHAMBA HERBAL PRODUCTS

A.J.T.C

A.J.T.C
ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE
Showing posts with label HABARI ZA BIASHARA. Show all posts
Showing posts with label HABARI ZA BIASHARA. Show all posts

Thursday, 4 December 2014

FANIKIWA KIBIASHARA

Siri ya kufanikisha biashara yako

Kama mwanzo wa makala ya hivi punde ya African Dream,mwanabiashara Mercy Kitomari-ambaye alianzisha kampuni ya kutengeza aiskrimu hai ya Nelwa's Gelato-anaeleza mbinu kumi bora anazotumia katika kuuza kwenye mitandao ya kijamii kwa wanabiashara chipukizi:
Anza na Lengo. 
Kuna majibu matatu pekee yanayokubalika: a)kuongeza kujulikana kwa bidhaa zako kwa kufikia watu zaidi b)kujenga imani ya wateja kwa kuwapa usaidizi zaidi ama c)kuongeza mauzo kwa kutafuta wanunuzi zaidi,watakaonunua mara kwa kwa mara.Usianze kama huwezi jibu swali hili.
Wapuuze wapinzani wako- Kujaribu kuiba wateja wa watu wengine ni mbinu mbovu.Utaanza kuunda maamuzi mabaya kwa sababu unajaribu kuwafikia.
Fikra na kampeni bora zaidi bado hazijatendeka katika sekta yako.Angalia nafasi ambazo hazijaguzwa unazoweza kupata na kutumia.Tazama kile watu wanafanya kwenye sekta tofauti na ujaribu mbinu hizo.
Usiwe kwenye mitandao yote ya kijamii.
Usimamizi wa kijamii utamaliza rasilmali zako zote.Kila mtandao wa kijamii unaosimamia utakugharimu muda,pesa na nguvu zaidi,kwa hivyo amua zile utazipa kipao mbele.


Una pesa na wakati wa kutosha.
Watu huwa wanasema kuwa hawana muda na pesa za kuwekeza katika mitandao ya kijamii.Lakini ukweli wa mambo ni kuwa hauwezi kutowekeza.Kama hauna fedha za kutosha,inafaa uwe na wakati zaidi wa kuunda maudhui ama kuunda mtandao.
Mercy Kitomari ana mkahawa wa Nelwa's Gelato mjini Dar es Salaam inayosambaza kwenye hoteli na biashara zingine.
Weka lengo rahisi-
Kwa mfano,kuchapisha mara mbili zaidi kila wiki-ama kufikia bloga mmoja kwa siku.Pia fanya ukaguzi wa ndani kujua jinsi unavyotumia muda wako kwa sasa.
Mitandao ya kijamii ni bora,lakini watu wengi huchanganya kushikika na kazi na kuwa na ufanisi.Tambua shughuli zinazoleta ''mapato kutoka kwa uwekezaji'' ya juu zaidi,zipe kipao mbele na uweke mipaka.
Kuwa na nidhamu na kuwajibika kwa wengine.
Mwishowe,utahitajika kuchukua msimamo mgumu.Utahitaji kugawanya rasilmali zako chache na kuchagua kile utakachofanya (na kile utakachopuuza).Lakini utaona kuwa uamuzi huu ni rahisi kama una lengo.Matumizi yako ya mitandao ya kijamii yatakuwa na kusudi.Utapata kuwa una wakati wa kutosha wa kuitumia kimkakati.
Tambua kile kinachohamasisha wasikilizaji wako.
''Sekta'' ama ''biashara'' hazichoshi-watu wanaosema hayo ndio wanaochosha.Jinsi unavyojenga mawazo ya maudhui ya blogi ni kuelewa wasikilizaji wako na faida ambazo bidhaa na huduma zako zinawapa.
Mercy Kitomari anasema kuwa huduma ya wateja ni muhimu sana kwenye mitandao sawia na ya uso kwa uso.
Kuwa na sauti.
Watu hawapendi kuungana na mashirika yasiyokuwa na uso.Wanataka kuungana na wanadamu wa kweli.Hakuna atakayiependa,amini ama kuheshimu kampuni yako ikiwa hawezi kupata majibu yaliyo sawa na yenye uaminifu kwa wakati ufaao.Mitandao ya kijamii ni zaidi ya ''kujiingiza katika mazungumzo''.Ni njia mpya ya kufanya mambo,na vifaa kadhaa vipya kukusaidia kufanya hivo.
Lakini misingi ya njia za mauzo inabakia.Unahitaji kuvutia watu,kujenga imani yao na kuwawezesha kushiriki zaidi.
Tamba sana kupitia Facebook na Twitter.Mitandao ya kijamii na mauzo kwenye mtandao inaanza na DNA yako,bidhaa ama huduma zako,na watu wako.Kwa hivyo kama unataka kuimarisha majibu yako kwenye mitandao ya kijamii,anda na kushughulikia utenda kazi wa ndani wa kampuni yako.Habari na VERONICA MRAMBOAH.chanzi bbc swahili

Wednesday, 3 December 2014

HABARI PICHA.UJASIRIA MALI ARUSHA


       Mwanamke mjasiriamali akiwa katika eneo lake la biashara yake jijini Arusha.  picha na Ombeni Pele}

Monday, 1 December 2014

MAKALA YA UCHUMI: UFUGAJI NYUKI UMEWAKOMBOA WASOMI KIUCHUMI






Wakiwa wanatengeneza mizinga ya kufugia nyuki mkoani Singida

Vijana wa kikundi cha Singida Youth Interprises and consultant cooperative society ambao ni wahitimu wa vyuo wanaojishughulisha na biashara ya ufagaji nyuki na uuzaji wa asali na nta


kijana Hamza Rajabu wa kikundi cha Singida Youth Interprises and consultant cooperative society ambao ni wahitimu wa vyuo wanaojishughulisha na biashara ya ufagaji nyuki na uuzaji akiwa kwenye maonyesho ya kongamano la ufugaji nyuki lililofanyika jijini Arusha hivi karibuni 


Na Ferdinand Shayo.Arusha.
Baada ya kuhitimu elimu ya chuo kikuu safari inaanza ya kuelekea kwenye jamii na kuanza maisha ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto zake ikiwemo suala la ajira ambalo ni suala mtambuka kwa kila mhitimu wa chuo.
Katika harakati za kufanya shughuli za kujiingizia kipato na kutengeneza ajira ,vijana 13 wa mkoa wa Singida ambao wote ni wahitimu kutoka vyuo mbali mbali wanakusanyika na kuanza kufuga nyuki pamoja na kuuza mazao ya nyuki ambayo ni asali,nta na sumu ya nyuki ambayo ni dawa.
Baada ya kuona fursa iliyopo katika sekta ya nyuki wanaamua kuitumia vyema kwa kuanza kufuaga nyuki na kuuza mazao yake ambayo yamewapatia faida za kiuchumi pamoja na kufanikiwa kuuza katika masoko ya nje.
Vijana hao walipohitimu chuo kikuu walijikusanya na kuunda kikundi cha Singida Youth Interprises and consultant cooperative society.
Mmoja wa wanachama wa kikundi hicho ni Hamza Rajabu anaeleza kuwa walianza kufuga nyuki wakiwa wenyewe baadae  wakaungana na vyama vya wafugaji nyuki ambapo tulivuna tani nyingi na kuiuza hadi soko la nje.
Hamza anaeleza kuwa changamoto kubwa iliyokua inawakabili ni ubora wa vifungashio (parking na lebel) lakini waliitatua kwa kupata mafunzo kutoka kwa wataalamu hivyo kufanikiwa.
Kama wahitimu tumefanikiwa kutengeneza vikundi 16 vya wafugaji nyuki na kuwapa ushauri wa kitaalamu,kutengeneza mabanda na vifaa bora vya kuchuja asali.
‘Binafsi nimehitimu chuo cha kilimo SUA mwaka juzi ,tunachokiona hapa kwenye sekta ya nyuki ni wajasiriamali wengi kukosa kuthibitishwa viwangoi na  TBS na  pia kupata vifungashio vizuri.  
Msimu uliopita tulizalisha tani 8 za asali na nta tani 18 kwa Mwekezaji kutoka Marekani .
Wahitimu wao ni kutoka vyuo mbali mbali ikiwemo  Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ,St.Agustine University (SUA).
Tunafanya biashara ya kuuza makundi ya nyuki katika sehemu mbali mbali ndani na nje ya Singida ,maeneo ya Nyumba ya nyuki na Iringa.
Wasomi hao wamefanikiwa kutengeneza makundi ya vijana,wazee na kinamama yanayojishughulisha na ufugaji nyuki.
Makundi hayo tunayapa mizinga miwili miwili kama mtaji ambao hutolewa na Mwekezaji kutoka nje kama mkopo wakivuna asali wanamuuzia mwekezaji huyo baada ya miaka miwili wanabaki na mizinga hiyo.
Mizinga inayotolewa ni ile ya kisasa ambayo huuzwa kiasi cha shilingi 65000 huwasaidia wafugaji kutunza asali nyingi ambayo wanaiuza na kuwapatia kipato.
Wakati mwingi tunatoa elimu kwa wafugaji nyuki namana ya kufanya ufugaji wa kisasa na kuvuna asali kwa kuzingatia usafi ,asali ambayo tunaiufungasha na kuiuza ndani na nje ya nchi.
Kwa sasa wanamiliki mashamba matatu ,moja kwa ajili ya kufuga makundi ya nyuki na kuyauza mengine ni kwa ajili ya asali,nta na sumu ya nyuki.
“Tuna mashamba matatu makubwa tunayatumia katika shughuli ya ufugaji kuku ,mawili yako Kisaki na moja liko wilaya ya Ikundi mkoani Singida.
Tunawashauri Watanzania na wasomi wenzetu wanaohitimu vyuo kutumia fursa lukuki zilizoko katika jamii zao na kujiajiri badala ya kusubiria kuajiriwa.
0765938008

Wednesday, 12 November 2014

Wataalamu wa Nishati na Madini watakiwa kuwa wabunifu.

 
NA FONIA BUNDALA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge amewasihi Watanzania kutumia teknolojia mpya  na za kisasa katika kuzalisha mazao na sekta nzima ya kilimo kwa ujumla ili kuzuia uharibifu wa mazingira ikiwemo misitu
.
Aliyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Ukuaji wa Uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi. Lililofanyika jijini Dar Es Salaam.
Alifungua Kongamano hilo kwa Niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Gharib Bilal.

Aliongeza kuwa Mikoa na Wilaya zote Tanzania  zinatakiwa kuweka sera endelevu ambazo zitaweza kuhakikisha kukabiliana na uharibifu wa Mazingira
.
Aidha alisema kuwa zipo juhudi ambazo Serikali imezichukua katika  kuhakikisha utunzaji wa  mazingira unatekelezwa na pia  kuzuia uharibifu wa mazingira kwa njia moja au nyingine.

Akiongea katika Kongamano hilo Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania Philippe Dongier alisema Kongamano hilo ni fursa adhimu kwa ajili ya majadiliano kuhusu program za maendeleo ya Tanzania zinavyoweza kustawi licha ya kuwepo kwa mabadiliko ya tabia Nchi. Hivyo basi Watanzania hawana budi kuwa waangalifu sababu mabadiliko ya Tabia Nchi yana athari kubwa.

AJTC

AJTC
ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLEGE