Pages

MUHAMBA

MUHAMBA
MUHAMBA HERBAL PRODUCTS

A.J.T.C

A.J.T.C
ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE
Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Monday, 17 November 2014

Prof Maghembe asema urais si mashindano ya urembo

 Habari na; ELIETH MTAITA
Waziri wa Maji, Prof Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari

Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe ameshangazwa na utitiri wa watu wanaotaka kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2015, akisema nafasi hiyo ya juu nchini haifanani na mashindano ya urembo ambayo mtu yeyote anaweza kujaribu.

Mbunge huyo wa Mwanga alisema watu hao wanaojitokeza kuwania urais hawaelezi wanataka kulifanyia nini Taifa na akashauri wasioweza kueleza hoja zao wasichaguliwe kushika nafasi hiyo.

“Urais unahitaji kuwa na sifa, dira na ajenda kwa Taifa,” alisema Profesa Maghembe wakati wa mahojiano maalumu na gazeti hili mjini hapa.

Kauli ya Profesa Maghembe imekuja wakati Taifa likijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, 2015, huku chama chake, CCM kikikabiliwa na kazi ngumu ya kumpata mrithi wa Rais Jakaya Kikwete ambaye anamaliza muda wake.

Hali kama hiyo iliikumba CCM wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 wakati takriban watu 20 walipojitokeza kutaka kuingia Ikulu na baadaye mwaka 2005 wakati wa uchaguzi uliomuweka madarakani Rais Kikwete.

Ndani ya CCM, mjadala huo sasa umekumbwa na hoja ya umri baada ya makada vijana kujitokeza kutangaza nia ya kumrithi Rais Kikwete kupambana na wanasiasa wakongwe, baadhi wakiwa ni wale waliojiandaa kwa muda mrefu.

Hata hivyo, Profesa Maghembe alipuuza mjadala huo wa umri wa mtu kugombea urais akisema kuwa hauna msingi na kwamba sifa kuu ya mgombea urais ni ajenda ya kuliletea Taifa maendeleo endelevu.

“Umri hauwezi kuleta tofauti katika uongozi wa nchi. Ni kama kusema jiwe liwe rais,” alisema mwanasiasa huyo mkongwe, ambaye amefanya kazi wizara tofauti tangu Januari 2006 aliposhika uwaziri kwa mara ya kwanza.

Alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inataka mgombea urais awe na umri wa kuanzia miaka 40 na kuendelea.

“Hivyo haisemi kuwa ukishakuwa na miaka 70 huwezi kuwa rais ama haisemi ukiwa na miaka 40 unafaa zaidi kuwa rais. Inategemea huyo mtu anayegombea anataka kuwafanyia nini Watanzania,” alisema.

Waziri huyo wa saba tangu Wizara ya Maji ianzishwe, alisema kugombea urais kunategemea ajenda aliyonayo mtu na hata watu wanapokwenda kumchagua, lazima waangalie ana ajenda gani. “Ikulu si mahali pa kukimbilia, mimi hata sijui wanakimbilia nini kwa sababu lazima mtu uwe na ajenda. Na kama mnasikia mtu anasema mimi nataka kuwa tu rais, huyo hafai kabisa,” alisema.

“Lazima mtu anayetaka kuwa rais atueleze uchumi sasa unakua kwa asilimia saba na umekuwa hivi kwa karibu miaka 10 lakini ni jambo linalofanya umaskini uwe mkali kabisa na usiishe ni kutokana na shughuli inayofanywa na watu wengi ya kilimo, kuwapatia kipato haikui kama sekta nyingine.

Chanzo; MWANANCHI COMMUNICATIONS

Wednesday, 12 November 2014

MBOWE AICHAKAZA MIKOA YA KIGOMA NA KATAVI

  NA: GIFTSILVANO MSANGI


Akinamama wa kijiji cha Igalula mkoani Kigoma, wakicheza ngoma ya asili, wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (kushoto), baada ya kuwasili kijijini hapo, ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Wananchi wa kijiji cha Igalula mkoani Kigoma, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wakati alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwakabidhi kadi za Chadema waliokuwa viongozi wa CCM wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga katija jimbo la Mpanda Vijijini, baada ya kujiunga na Chadema katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Badhii ya waliokuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga katika jimbo la Mpanda Vijijini, wakimkabidhi kadi za CCM Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, walipoamua kujiunga na Chadema, baada ya mkutano wa Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kijijini Hapo juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisalimiana na Bi. Mariamu Ramadhani (86), baada ya kuwasili katika kijiji cha Kapalamsenga mkoani Katavi, ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Zanzibar), Salumu Mwalimu akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Waliokuwa viongozi wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga kupitia CCM, wakionyesha kadi zao kabla ya kuzikabidhi kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, walipojiunga na chama hicho wakati wa mkutano wa Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kijiji hapo juzi.

WABUNGE WATAKIWA KUTANGAZA MALI ZAO PINDI WANAPO STAAFU

NA GLORI CHACKY
Mbunge wa Viti Maalum, Amina Abdullah Amour (CUF), ameitaka itunge sheria ya kuwataka viongozi wa umma kuorodhesha mali zao wanapostaafu ili kujua ni mali walizopata wakati wa uongozi wao.


 Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Nchi

MREMA APOKELEWA KWA KISHINDO NA WANANCHI WA JIMBO LAKE

NA: GASPER MUSHI
Mkutano wa hadhara wa chama cha Tanzania Labour (TLP) uliokuwa ukihutubiwa na Mbunge wa jimbo la Vunjo Agustine Mrema jirani na matanki ya Maji katika kijiji cha Mieresini wilaya ya Moshi vijijini.
Afisa uhusiano wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Frolah Nguma (aliyesimama)akitoa ufafanuzi juu ya maswala ya maji baada ya Mbunge Mrema kumtaka kufanya hivyo muda mfupi baada ya maofisa wa Mamlaka hiyo kufika katika Matenki ya Maji kwa ajili ya ukaguzi wa kawaida.
Msimamizi mkuu wa (MUWSA) Kituo cha Himo Brucevictor Sangawe akitoa ufafanuzi kwa wananchi mbele ya mbunge wa jimbo la Vunjo ,Agustine Mrema juu ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo ya ukanda wa juu katika mji wa Himo.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Mbunge Mrema.
Mh Mrema akifuatilia maelezo ya maofisa wa Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) walipokuwa wakitoa maelezo kwa wananchi (hawapo pichani)  ,Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya kasakazini.

AJTC

AJTC
ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLEGE