Pages

MUHAMBA

MUHAMBA
MUHAMBA HERBAL PRODUCTS

A.J.T.C

A.J.T.C
ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE

Monday, 17 November 2014

Ebola yamfukuzisha kazi Waziri wa Afya wa Liberia


Habari na:Francis L. Matana:
Ebola yamfukuzisha kazi Waziri wa Afya wa Liberia

Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia amemfukuza kazi Walter Gwenigale Waziri wa Afya wa nchi hiyo na nafasi yake itachukuliwa na George Warner aliyekuwa mkuu wa zamani wa huduma za umma. 

Taarifa kutoka Monrovia zinasema kuwa, Walter Gwenigale amefutwa kazi kutokana na kushindwa kukabiliana na kasi ya homa ya ebola iliyotikisa nchini humo. 

Hata hiyo taarifa kutoka Ofisi ya Rais ya Liberia inaeleza kuwa, Gwenigale ataendelea kuwa mshauri wa Rais katika Kamati ya Ebola hadi atakapostaafu kwenye utumishi wa umma mwezi Februari mwakani.


Rais Sirleaf amelifanyia pia marekebisho madogo baraza la mawaziri kwa kuwateuwa mawaziri wapya wa elimu,huduma za umma na mkuu wa  kituo cha taifa cha redio.

Ripoti ya Shirika la Afya Duniani imetangaza kuwa, zaidi ya watu 2,800 wamefariki dunia nchini Liberia kati ya watu 5,147 waliofariki dunia kutokana na maradhi ya ebola barani Afrika

Chanzo:Radio Tehran

0 comments:

Post a Comment

AJTC

AJTC
ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLEGE