Luke Somers raia wa Marekani mwandishi wa habari anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda huko Yemen
Na JASMINE MUMWI.
Marekani imeeleza kuwa ilijaribu
kumwokoa raia wake mzaliwa wa Uingereza Luke Somers, anayeshikiliwa
mateka na al-Qaeda nchini Yemen.
Rais Barack Obama aliidhinisha kikosi cha kumwokoa Luke, mwezi uliopita.
"Kwa
masikito, Luke hakuwepo, japokuwa mateka kutoka mataifa mengine
walikuwepo na waliokolewa," Baraza la Usalama la Taifa, limesema.
Mtu
anayejitambulisha kama Luke Somers, ambaye alitekwa mwaka 2013,
ameonekana katika video, akisema maisha yake yako hatarini na anaomba
msaada.
Video hiyo pia inamwonyesha mfuasi wa al-Qaeda huko Yemen
akitishia kumuua Bwana Somers hadi madai yao ambayo hayajatajwa,
yatakapotimizwa.
Bwana Somers, mwenye umri wa miaka 33,
alifanyakazi kama mwandishi wa habari na mpiga picha wa mashirika ya
huko na kazi zake zikaonekana katika vyombo vya habari vya kimataifa,
ukiwemo mtandao wa BBC.
CHANZO. BBC SWAHILI.
Rais Robert Mugabe awalaumu baadhi ya wapinzani
wake ndani ya chama cha ZANU PF kwa kupanga kumuondoa mamlakani
Na JASMINE MUMWI.
Rais
wa Zimbabwe Robert Mugabe amelaumu baadhi ya watu ndani ya chama chake
tawala cha ZANU-PF kwamba wanapanga kumng'oa madarakani.
Akizungumza
katika kongamano la chama hicho, Mugabe amesema amebaini kuwepo
majaribio ya kuwahonga wajumbe kumpinga kama kiongozi, lakini
akasisitiza wajumbe hawawezi kupokea hongo.
Wanachama wengi wa chama hicho wangali ni wafuasi sugu wa Rais Mugabe
Mugabe ameahidi
kupambana na rushwa ndani ya chama na kukabiliana na maafisa wa chama
hicho ambao kazi yao ni kutoa hongo na kupokea rushwa.
Hasira ya Mugabe ilionekana
kufuatia madai ya njama ya kutaka kumuua yanayodaiwa kuandaliwa na
naibu wake Joyce Mujuru. Hata hivyo Mujuru alikanusha madai hayo ambayo
yamekuwa yakimuandamana.
Mugabe alisema kutokuwepo kwa Bi Mujuru kwenye mkutano huo wa chama kunaonyesha kuwa anaogopa.
Maelfu ya wajumbe wa chama walihudhuria kongamano hilo mjini Harare
Kadhalika Mugabe amesema Mujuru ni mwizi anayepanga kumuondoa mamlakani kwa kushirikiana na maafisa wengine wa chama. Chama tawala cha Zimbabwe
kinakumbwa na vita vya ndani kwa ndani kuhusiana na nani atarithi nafasi
ya Mugabe ambaye ana miaka 91 na ambaye ameongoza tangu uhuru wa taifa
hilo. Hata hivyo amekanusha madai ya kwamba anataka kujiuzuru na kusema kuwa huo ni upuuzi. Hivi
karibuni afisa mwingine mkuu wa chama tawala, Robert Gumbo aliiambia
BBC kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 90 amegeuza chama tawala na
kukifanya kama mali yake binafsi. Gumbo alisema lengo kuu la Mugabe ilikuwa kuendeleza uongozi wa chama kwa niaba ya mke wake Grace. Bi
Mujuru ambaye amekanusha madai hayo alionekana kama mtu ambaye
anechukua usukani wa chama kutoka kwa Mugabe ambaye walipigania naye
uhuru wa nchi hiyo kutoka mikononi mwa watwala wazungu. chanzo; BBC SWAHILI
Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imempa kiongozi wa mashtaka katika mahakama hiyo Fatou Bensouda muda wa wiki moja ili kutoa ushahidi dhidi ya rais wa Kenya, la sivyo aondoe mashtaka dhidi yake.
''Kucheleweshwa kwa kesi hiyo ya Rais Uhuru ni kinyume na maslahi ya haki.'' ilisema.Rais Kenyatta ni kiongozi wa kwanza wa taifa kufika katika mahakama hiyo tangu ashtakiwe rasmi mwaka 2012 na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu,ambayo ameyakana.Kiongozi huyo wa mashtaka ametaka kupewa muda zaidi ili kujenga kesi yake dhidi ya kiongozi huyo.Anasema kwamba mashahidi wamehongwa na kutishiwa maisha huku serikali ya Kenya ikikataa kutoa stakhabadhi muhimu za kesi hiyo.Bwana Kenyatta amekanusha kuchochea ghasia kufuatia mgogoro wa uchaguzi wa mwaka 2007 ili kumpatia ushindi aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki na kusema kuwa kesi hiyo ni ya kisiasa.
Akikataa ombi la kiongozi huyo wa mashtaka kuchelewesha kesi hiyo, majaji wa mahakama hiyo walisema kuwa wamempatia wiki moja Bensouda kusema iwapo ataitupilia mbali kesi hiyo ama ushahidi alio nao unaweza kuhimili kesi hiyo kuendelea.Rais Kenyatta alishinda uchaguzi wa urais mwaka 2013 kupitia usaidizi wa Mwai Kibaki.Aliitumia kesi hiyo kutafuta kuungwa mkono huku akiikashifu mahakama hiyo ya mjini Hague kwa kuingilia masuala ya Kenya.Ameshtakiwa na mahakama hiyo kwa kuhusika moja kwa moja katika mauaji ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008.Takriban watu 1,200 waliuawa katika ghasia hizo huku wengine 600,000 wakiachwa bila makazi.habari na JASMINE R MUMWI CHANZO BBC SWAHILI
Nahodha wa Manchester united Wayne Rooney, atafanyiwa uchunguzi zaidi ili kujua ukubwa wa tatizo la goti lake.
Rooney 29 aliukosa mchezo wa jana dhidi ya Stoke City uliomalizika kwa man united kupata ushindi wa 2 kwa 1, jeraha hili la goti alilipata katika dakika za mwisho za mchezo mwa ligi kuu ulofanyika jumamosi iliyopita kwenye mchezo na Hull City.
Meneja Louis van Gaal, amesema, "atafanyiwa uchunguzi zaidi na imani jeraha sio kubwa hivyo ila tunasubiri majibu ya uchunguzi”.
Bosi huyo wa man united anaamini Rooney na Di maria hawawezi kuwa fiti kuweza kuwakabili Southampton,
United imekua ikiandamwa na majeruhi wengi tangu kuanza kwa msimu huu ambako nyota wake kadhaa bado wako bechi kwa majeruhi.habari na veronica mramboah..bbc
Nchini Tanzania kuna maeneo machache ambayo baadhi ya watu wake hawana uelewa thabit wa kutumia mipira ya kiume(Condoms) kiasi ambacho mpira mmoja unaweza kutumiwa na vijana watatu hadi wanne kwa kubadilishana baada ya kuusafisha na kuanika juani.Hali hiyo imeelezwa kuwa chanzo kingine cha kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza alitembelea wilaya ya Longido kaskazini mwa Tanzania kijijini Orglay na kuzungumza na mmoja kati ya vijana wa kijiji hicho.HABARI NA VERONICA MRAMBOAH. BBC SWAHILI
Kama mwanzo wa makala ya hivi punde ya African Dream,mwanabiashara Mercy Kitomari-ambaye alianzisha kampuni ya kutengeza aiskrimu hai ya Nelwa's Gelato-anaeleza mbinu kumi bora anazotumia katika kuuza kwenye mitandao ya kijamii kwa wanabiashara chipukizi:
Anza na Lengo.
Kuna majibu matatu pekee yanayokubalika: a)kuongeza kujulikana kwa bidhaa zako kwa kufikia watu zaidi b)kujenga imani ya wateja kwa kuwapa usaidizi zaidi ama c)kuongeza mauzo kwa kutafuta wanunuzi zaidi,watakaonunua mara kwa kwa mara.Usianze kama huwezi jibu swali hili.
Wapuuze wapinzani wako- Kujaribu kuiba wateja wa watu wengine ni mbinu mbovu.Utaanza kuunda maamuzi mabaya kwa sababu unajaribu kuwafikia.
Fikra na kampeni bora zaidi bado hazijatendeka katika sekta yako.Angalia nafasi ambazo hazijaguzwa unazoweza kupata na kutumia.Tazama kile watu wanafanya kwenye sekta tofauti na ujaribu mbinu hizo.
Usiwe kwenye mitandao yote ya kijamii.
Usimamizi wa kijamii utamaliza rasilmali zako zote.Kila mtandao wa kijamii unaosimamia utakugharimu muda,pesa na nguvu zaidi,kwa hivyo amua zile utazipa kipao mbele.
Una pesa na wakati wa kutosha.
Watu huwa wanasema kuwa hawana muda na pesa za kuwekeza katika mitandao ya kijamii.Lakini ukweli wa mambo ni kuwa hauwezi kutowekeza.Kama hauna fedha za kutosha,inafaa uwe na wakati zaidi wa kuunda maudhui ama kuunda mtandao.
Mercy Kitomari ana mkahawa wa Nelwa's Gelato mjini Dar es Salaam inayosambaza kwenye hoteli na biashara zingine.
Weka lengo rahisi-
Kwa mfano,kuchapisha mara mbili zaidi kila wiki-ama kufikia bloga mmoja kwa siku.Pia fanya ukaguzi wa ndani kujua jinsi unavyotumia muda wako kwa sasa.
Mitandao ya kijamii ni bora,lakini watu wengi huchanganya kushikika na kazi na kuwa na ufanisi.Tambua shughuli zinazoleta ''mapato kutoka kwa uwekezaji'' ya juu zaidi,zipe kipao mbele na uweke mipaka.
Kuwa na nidhamu na kuwajibika kwa wengine.
Mwishowe,utahitajika kuchukua msimamo mgumu.Utahitaji kugawanya rasilmali zako chache na kuchagua kile utakachofanya (na kile utakachopuuza).Lakini utaona kuwa uamuzi huu ni rahisi kama una lengo.Matumizi yako ya mitandao ya kijamii yatakuwa na kusudi.Utapata kuwa una wakati wa kutosha wa kuitumia kimkakati.
Tambua kile kinachohamasisha wasikilizaji wako.
''Sekta'' ama ''biashara'' hazichoshi-watu wanaosema hayo ndio wanaochosha.Jinsi unavyojenga mawazo ya maudhui ya blogi ni kuelewa wasikilizaji wako na faida ambazo bidhaa na huduma zako zinawapa.
Mercy Kitomari anasema kuwa huduma ya wateja ni muhimu sana kwenye mitandao sawia na ya uso kwa uso.
Kuwa na sauti.
Watu hawapendi kuungana na mashirika yasiyokuwa na uso.Wanataka kuungana na wanadamu wa kweli.Hakuna atakayiependa,amini ama kuheshimu kampuni yako ikiwa hawezi kupata majibu yaliyo sawa na yenye uaminifu kwa wakati ufaao.Mitandao ya kijamii ni zaidi ya ''kujiingiza katika mazungumzo''.Ni njia mpya ya kufanya mambo,na vifaa kadhaa vipya kukusaidia kufanya hivo.
Lakini misingi ya njia za mauzo inabakia.Unahitaji kuvutia watu,kujenga imani yao na kuwawezeshakushiriki zaidi.
Tamba sana kupitia Facebook na Twitter.Mitandao ya kijamii namauzo kwenye mtandao inaanza na DNA yako,bidhaa ama huduma zako,na watu wako.Kwa hivyo kama unataka kuimarisha majibu yako kwenye mitandao ya kijamii,anda na kushughulikia utenda kazi wa ndani wa kampuni yako.Habari na VERONICAMRAMBOAH.chanzi bbc swahili
Wanafunzi katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakishiriki mashindano ya riadha yaliyoandaliwa chuoni hapo katika kiwanja cha fidifosi. Picha na; FRANCIS MATANA
Wanariadha wa timu ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakiwa katika mazoezi yao ya kawaida kwenye viwanja vya jeshi la kutuliza ghasia. Picha na Elieth Mtaita
Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) Bi NEEMA MWAIPELA akizungumza machache kabla ya mahafali ya tisa ya chuo hicho kuanza, yaliyofanyika katika ukumbi wa PPS Ijumaa mkoani Arusha. ( Picha na Edilitruda Chami)
katika picha ni baadhi ya wahitimu wa chuo cha uandishi wa habari na utanganzaji Arusha wakiwa na mgeni rasmi alie kaa wapili kushoto pamoja na wakufunzi wao. picha na Christina Kilovele
Mgeni rasmi katika mahafali ya 9 katika chuo cha Uandishi wa habari na utangazaji Arusha{bw.Fredrick Mumbuli kulia}akitunukiwa cheti cha heshima na kaimu mkuu wa chuo hicho bw Elifuraha Samboto hivi karibuni.Picha na Lydia Kishia.
Msanii wa HIP HOP SIDE TONIC Akitumbuiza katika ukumbi wa kukutania wanafunzi katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) Kabla ya kuanza kwa mashindano ya Utangazaji kati ya chuo hicho na chuo cha Habari Maalumu
Wakufunzi katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi kwenye mahafali ya tisa ya chuo hicho. (Picha na Glory Chacky)
Mwajuma abdul Akisoma Risala maalumu kwa mgeni rasmi katika mahafali ya Tisa ya chuo cha uandishi wa habari Na Utangazaji Arusha (AJTC) yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PPS
baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wakiwa kwenye mahafali ya tisa katika ukumbi wa PPS jijini Arusha. PICHA NA SINYATI KILUSU.
Mhitimu wa ngazi ya Diploma katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bi MERLINE OLOTU Akikata keki katika hafra fupi baada ya Mahafali iliyofanyika katika ukumbi wa PPS
wanafunzi wa darasa la AICC katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha bw. Sebastian Mnakaya(aliekaa)na bw.Bugoma wa Bugoma wakituma habari kwa njia ya mtandao mapema leo chuoni hapo.
Wanafunzi wa chuo cha uandishi habari na utangazaji Arusha wakifuatilia uwasilishaji wa somo katika ukumbi wa chuo hicho. (Picha na Emma Moshi)
Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. ONESMO ELIA MBISE akitoa hitimisho baada ya uwasilishwaji wa somo chuoni hapo hivi karibuni. (Picha na Mbonea E. Daniel)
Makamu mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. ELIFURAHA JOHN SAMBOTO akifurahia jambo wakati wa uwasilishwaji wa somo chuoni hapo. (Picha na Giftsilvano Msangi)
Mwanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na tangazaji Arusha, Mwanahawa Kitomari akifanya uwasilishaji wa somo chuoni hapo. (Picha na Veronica Mramboah)
Mgeni rasmi katika mahafali ya tisa ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Fredrick Mumbuli ambaye amesimama katikati akihutubia katika mahafali hayo ambayo yalifanyika tarehe 28 mwezi wa 11 mwaka huu katika ukumbi wa PPS jijini Arusha. PICHA NA ESTHER A. CHAVALA
Wahitimu wa chuo cha uandishi wa habari na Utangazaji Arusha AJTC wakiwa katika mahafali ya tisa ya kuhitimu masomo yao ya ngazi ya stashada yaliyofanyika tarehe 28 mwezi 11 mwaka huu katika ukumbi wa PPS jijini Arusha. PICHA NA FONIA BUNDALA.
Dokta Hamisi Kigwangala akilakiwa na waumini wa kanisa la KKKT Olorieni jijini Arusha Hivi karibuni
Dokta Kigwangalla akihojiwa na mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi Mussa Juma juu ya suala la Escrow account
Dokta Kigwangallah akitoa nasaha kwa wananakwaya wa kwaya ya Msifuni iliyozindua albamu yao ya Video hivi karibuni katika kanisa la KKKT Olorieni jijini Arusha hivi karibuni
Mheshimiwa
Hamissi Kigwangalla akivishwa vazi la heshima la kimaasai kabla ya
kuingia kanisani ili kufanya uzinduzi wa DVD ya kwaya ya MSIFUNI ya
kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania usharika wa Olorieni jijini A
rusha mapema leo
Mtangazaji
maarufu wa radio living water ya jijini Mwanza NEEMA NDULLU aliyekuwa
mshereheshaji wa tamasha la waimbaji lililofanyika jana katika kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania mtaa wa MARA usharika wa Olorieni jimbo
la kaskazini kati lililokuwa na nia ya kumuinua na kumsifu Mungu kwa
njia ya uimbaji
Mwimbaji
wa nyimbo za injili Peter Mwabulambo akiwapa burudani ya aina yake
katika tamasha la waimbaji wa nyimbo za injili lililofanyika katika
kanisa la KKT olorieni jana jioni
Vijana wa EZEKIEL VISION wakimsifu na kumtukuza MUNGU katika tamasha hilo
Mwibaji Abednego wa nyimbo za injili na timu yake wakiwaburudisha waumini waliohudhuria tamasha hilo la nyimbo za INJILI
Wakiwa wanatengeneza mizinga ya kufugia nyuki mkoani Singida
Vijana wa kikundi cha Singida Youth Interprises and
consultant cooperative society ambao ni wahitimu wa vyuo wanaojishughulisha na
biashara ya ufagaji nyuki na uuzaji wa asali na nta
kijana Hamza Rajabu wa kikundi cha Singida Youth Interprises
and consultant cooperative society ambao ni wahitimu wa vyuo wanaojishughulisha
na biashara ya ufagaji nyuki na uuzaji akiwa kwenye maonyesho ya kongamano la
ufugaji nyuki lililofanyika jijini Arusha hivi karibuni
Na Ferdinand Shayo.Arusha.
Baada ya
kuhitimu elimu ya chuo kikuu safari inaanza ya kuelekea kwenye jamii na kuanza
maisha ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto zake ikiwemo suala la ajira
ambalo ni suala mtambuka kwa kila mhitimu wa chuo.
Katika
harakati za kufanya shughuli za kujiingizia kipato na kutengeneza ajira ,vijana
13 wa mkoa wa Singida ambao wote ni wahitimu kutoka vyuo mbali mbali
wanakusanyika na kuanza kufuga nyuki pamoja na kuuza mazao ya nyuki ambayo ni
asali,nta na sumu ya nyuki ambayo ni dawa.
Baada ya
kuona fursa iliyopo katika sekta ya nyuki wanaamua kuitumia vyema kwa kuanza
kufuaga nyuki na kuuza mazao yake ambayo yamewapatia faida za kiuchumi pamoja
na kufanikiwa kuuza katika masoko ya nje.
Vijana hao
walipohitimu chuo kikuu walijikusanya na kuunda kikundi cha Singida Youth
Interprises and consultant cooperative society.
Mmoja wa
wanachama wa kikundi hicho ni Hamza Rajabu anaeleza kuwa walianza kufuga nyuki
wakiwa wenyewe baadae wakaungana na
vyama vya wafugaji nyuki ambapo tulivuna tani nyingi na kuiuza hadi soko la
nje.
Hamza
anaeleza kuwa changamoto kubwa iliyokua inawakabili ni ubora wa vifungashio
(parking na lebel) lakini waliitatua kwa kupata mafunzo kutoka kwa wataalamu
hivyo kufanikiwa.
Kama
wahitimu tumefanikiwa kutengeneza vikundi 16 vya wafugaji nyuki na kuwapa
ushauri wa kitaalamu,kutengeneza mabanda na vifaa bora vya kuchuja asali.
‘Binafsi
nimehitimu chuo cha kilimo SUA mwaka juzi ,tunachokiona hapa kwenye sekta ya
nyuki ni wajasiriamali wengi kukosa kuthibitishwa viwangoi na TBS na
pia kupata vifungashio vizuri.
Msimu
uliopita tulizalisha tani 8 za asali na nta tani 18 kwa Mwekezaji kutoka
Marekani .
Wahitimu wao
ni kutoka vyuo mbali mbali ikiwemo Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM) ,St.Agustine University (SUA).
Tunafanya
biashara ya kuuza makundi ya nyuki katika sehemu mbali mbali ndani na nje ya
Singida ,maeneo ya Nyumba ya nyuki na Iringa.
Wasomi hao
wamefanikiwa kutengeneza makundi ya vijana,wazee na kinamama yanayojishughulisha
na ufugaji nyuki.
Makundi hayo
tunayapa mizinga miwili miwili kama mtaji ambao hutolewa na Mwekezaji kutoka
nje kama mkopo wakivuna asali wanamuuzia mwekezaji huyo baada ya miaka miwili
wanabaki na mizinga hiyo.
Mizinga
inayotolewa ni ile ya kisasa ambayo huuzwa kiasi cha shilingi 65000 huwasaidia
wafugaji kutunza asali nyingi ambayo wanaiuza na kuwapatia kipato.
Wakati
mwingi tunatoa elimu kwa wafugaji nyuki namana ya kufanya ufugaji wa kisasa na
kuvuna asali kwa kuzingatia usafi ,asali ambayo tunaiufungasha na kuiuza ndani
na nje ya nchi.
Kwa sasa
wanamiliki mashamba matatu ,moja kwa ajili ya kufuga makundi ya nyuki na
kuyauza mengine ni kwa ajili ya asali,nta na sumu ya nyuki.
“Tuna
mashamba matatu makubwa tunayatumia katika shughuli ya ufugaji kuku ,mawili
yako Kisaki na moja liko wilaya ya Ikundi mkoani Singida.
Tunawashauri
Watanzania na wasomi wenzetu wanaohitimu vyuo kutumia fursa lukuki zilizoko
katika jamii zao na kujiajiri badala ya kusubiria kuajiriwa.