akielekea katika ofisi za kanisa hilo mara baada ya kufanya uzinduzi wa DVD ya kwaya ya MSIFUNU kanisani hapo mapema leo |
Hapa mgeni Rasmi Hamisi Kigwangalla akiwasihi waumini hao hawapo pichani juu ya kudumisha amani na Upendo miongoni mwa watu wa itikadi na dini tofauti ili uhuru wa kuabudu udumishwe nchini |
akiwashukuru wanakwaya wa kwaya ya MSIFUNI kwa kumpa heshima ya kipeke kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa DVD yao |
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Dokta Hamisi Kigwangala ambaye ni mbunge wa jimbo la Nzega na mwenyekiti wa kamati ya bunge inayosimamia TAMISEMI amewaasa wanakwaya wa kwaya ya MSIFUNI kuendelea kumtumikia Mungu kwa kuimba na kusifu ili amani upendo na ushirikiano miongoni mwa watanzania udumu milele.
Akizindua DVD ya kwaya ya MSIFUNI ya kanisa la KKT olorieni mapema leo amesema kuwa kazi ya kumtumikia Mungu ni ya kipekee kwani inalenga kuwajenga watu kiimani, kuleta ushirikiano na amani nchini Tanzania ambapo
katika uzinduzi huo aliwezesha kupatikana kwa jumla ya shilingi milioni 14
ambapo mchnganuo wa fedha hizo
fedha taslimu 2,965,400
ahadi ni 7,120,000/=Tshs
hundi 4,400,000/=Tshs
kati ya fedha hizo mheshimiwa Kigwangala alichangia jumla ya shilingi millionsita, ofisis ya mkuu wa m,koa wa Arusha shilingi millioni tano na mkuu wa wilaya ya Arumeru alichangia shilingi millioni moja na nusu na waumini mbalimbali walichangia sehemu iliyobaki
Hata hivyo hakusita kuelezea sakata la escrow account ambapo amemshukuru Mungu kwani limemalizika vema pasi na kuwagawa wananchi wa Tanzania ambapo alisema wameazimia kuwa mawziri wawili lazima waondolewe, katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini avuliwe wadhifa wake na mwanasheria mkuu wa serikali avuliwe nyadhifa zake na kufikishwa katika vyombo vya sheria na ikithibitika wametenda kosa wafilisiwe mali zao ili zirejeshwe kwa umma
amesisitiza kuwa haiwezekani mtu aibie watanzania halafu aachiwe huru na kuendelea na maisha yake pasi na kushtakiwa kwani itakuwa haijawasaidia watanzania.
alipoulizwa na wanahabari ni kwa nini hawajataka kumuajibisha waziri mkuu alisema kuwa katika ishu hii ya esrow account hakushiriki moja kwa moja kushinikiza au kupanga ubadhirifu huo wa fedha za uma na hivyo bunge kuazimia kutomchukulia hatua yoyote
0 comments:
Post a Comment