Balozi wa Nigeria nchini Marekani amekosoa msaada wa Washington katika vita dhidi ya Boko Haram na kusema kuwa hautoshi na kwamba Marekani i meshindwa kutoa taarifa za kutosha za kijasusi na kuzuia silaha zinazotakiwa katika mapambano dhidi ya kundi hilo la kigaidi.
Ade Adefuye ameitaka Washington itoe msaada zaidi kwa Nigeria na kutupilia mbali madai kwamba ukiukaji wa haki za binadamu umezuia baadhi ya misaada ya jeshi la Marekani.
Amesema kwamba, wananchi wa Nigeria hawaridhishwi na msaada unaotolewa na Marekani katika vita dhidi ya Boko Haram na kwamba hakuna maana ya kupewa msaada ambao haufanikishi lengo hilo.
Hayo yanajiri huku serikali ya Rais Goodluck Jonathan ikiendelea kukosolewa kwa kushindwa kulitokomeza kundi hilo linaloendelea kufanya mashambulizi dhidi ya raia nchini humo.
Licha ya ukosoaji huo Jonathan ametangaza rasmi nia yake ya kugombea tena katika uchaguzi ujao wa rais nchini Nigeria.
Chanzo; Radio Tehran
0 comments:
Post a Comment