Pages

MUHAMBA

MUHAMBA
MUHAMBA HERBAL PRODUCTS

A.J.T.C

A.J.T.C
ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE

Wednesday, 12 November 2014

Ebola:Wahudumu 400 wagoma Sierra Leone





 Habari na; DADU CHARLES
Takriban watu 5,000 wamefariki Afrika Magharibi kutokana na Ebola
Zaidi ya wahudumu 400 wa afya wanaowatibu wagonjwa wa Ebola katika kliniki moja nchini Sierra Leone wamegoma.

Wahudumu hao wakiwemo wauguzi na wafanyaki wengineo wamegoma na kulalamikia hatua ya serikali kukosa kuwalipa dola miamoja kila wiki kwa kuhatarisha maisha yao wakiwashughulikia wagonjwa wa Ebola.

Kliki hiyo iliyo mjini Bandajuma karibu na eneo la Bo, ndio kliniki pekee ambako wagonjwa wa Ebola wanatibiwa Kusini mwa Sierra Leone.

Nako nchini Mali, muuguzi mmoja  pamoja na mgonjwa aliyetibiwa na muuguzi huyo wamefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola.

Idadi hiyo inafikisha watu watatu waliofariki kutokana na Ugonjwa huo nchini humo
Mgonjwa alikuwa mwanamume mganga wa kiisilamu aliyekuwa na umri wa miaka 50 na alikuwa ameingia nchini humo kutoka Guinea.

Alitibiwa na muuguzi aliyefariki akiwa na umri wa miaka 25 mjini Bamako katika kliniki ya Pasteur ambayo kwa sasa imekfungwa na kuwekwa karantini.

Vifo hivi havijahusishwa na kifo cha mtoto mwenye umri wa miaka miwili aliyefariki kutokana na Ebola mwezi oKtoba.
Shirika la Afya Duniani limetangaza mlipuko huu wa Ebola kama janga la dunia.

Takriban watu 5,000 wamefariki kutokana na Ebola katika mataifa ya Afrika Magharibi hasa nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Chanzo; BBC

0 comments:

Post a Comment

AJTC

AJTC
ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLEGE