NA LILIAN REUBEN
Rais wa China Xi Jinping amesema
amefanya mazungumzo yenye tija na Rais wa Marekani Barack Obama na nchi hizo
mbili zimekubaliana kuharakisha mazungumzo kuhusu uwekezaji wa pamoja na
kuboresha uhusiano wa kijaeshi.
Rais Xi amesema China na Marekani
zimekubaliana kuchukua hatua za kuimarisha
uhusiano katika masuala muhimu
yatakayojenga imani kati yao kama ulinzi na ushirikiano katika kupambana na
ugaidi.
Nchi hizo mbili pia zimekubaliana
kuhusu ushirikiano wa kuimarishwa kwa sheria ikiwemo kukabiliana na uhalifu wa
kuvunjwa kwa sheria za kimataifa.
Marekani yasema iko tayari
kushirikiana na China
Rais wa Marekani Barack Obama
amesema licha ya Marekani na China kuwa washindani, miamba hao wawili wa
kiuchumi duniani wanaweza kufanya kazi kwa pamoja katika masuala
watakayokubaliana ili kuimarisha usalama wa raia wao.
Rais wa Marekani Barack Obama na
Rais wa China Xi Jinping
Xi na Obama wameyasema hayo hii leo
katika mkutano na wanahabari mjini Beijing, China baada ya mazungumzo ya siku
mbili kuhusu masuala ya kiuchumi na usalama kati yao.
Obama ametangaza katika mkutano huo
kuwa nchi yake itapunguza kiwango cha gesi chafu inayotoka viwandani na China
kwa upande wake imeahidi itachukua hatua madhubuti kupunguza gesi hiyo
inayoharibu mazingira kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyo sasa, hatua ambayo
imetajwa kuwa ya kihistoria kufuatia kujivuta kwa China kujitolea kufanya hivyo
katika kipindi cha nyuma.
Obama amesema hatua hiyo ni ufanisi
mkubwa katika uhusiano wa nchi hizo mbili na inaonyesha kile kinachoweza
kufikiwa iwapo zitashirikiana kushughulikia changamoto kubwa zinazoukumba
ulimwengu.
Tangazo hilo la kupunguza gesi chafu
kutoka viwandani kutoka China na Marekani ambazo ni miongoni mwa wachafuzi
wakubwa duniani wa mazingira zinaonyesha kujitolea kwa nchi hizo mbili katika
kushughulikia tatizo hilo ambalo limepandisha viwango vya joto duniani lakini
jinsi zitavyofikia shabaha hiyo bado inasubiriwa kuonekana itakuwa vipi.
Nchi zote mbili kupunguza uchafuzi
wa mazingira
Marekani imeweka malengo ya
kupunguza gesi hiyo kwa kati ya asilimia 26 hadi 28 ifikapo mwaka 2025
ikilinganishwa na viwango ilivyoviweka mwaka 2005 vya kuipunguza kwa asilimia
17 ifikapo mwaka 2020.
Gesi chafu ikitoka viwandani China
Aliyekuwa makamu wa Rais wa Marekani
Al Gore amelitaja tangazo hilo kama hatua kubwa katika kuelekea kuutatua mzozo
wa madhara ya mabadiliko ya hewa ulimwenguni.
Hata hivyo wanasiasa wa chama cha
Republican nchini Marekani wamesema watapinga mpango huo kwa hoja kwamba Obama
ataawachia marais wa siku za usoni nchini humo mzigo wa kulifikia lengo hilo
ambalo ni gumu mno.
Obama amegusia pia kuhusu umuhimu wa
watu wa Hong Kong kushiriki katika uchaguzi huru na wa haki huku Xi akisema
hilo ni suala la ndani la China kulishughulikia.
Viongozi hao wanatarajiwa baadaye
leo kuhudhuria mkutano wa kibiashara wa nchi za kusini mashariki mwa bara Asia
unaofanyika leo nchini Myanmar. chanzo dw swahili
S



0 comments:
Post a Comment