Luke Somers raia wa Marekani mwandishi wa habari anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda huko Yemen
Na JASMINE MUMWI.
Marekani imeeleza kuwa ilijaribu
kumwokoa raia wake mzaliwa wa Uingereza Luke Somers, anayeshikiliwa
mateka na al-Qaeda nchini Yemen.
Rais Barack Obama aliidhinisha kikosi cha kumwokoa Luke, mwezi uliopita.
"Kwa
masikito, Luke hakuwepo, japokuwa mateka kutoka mataifa mengine
walikuwepo na waliokolewa," Baraza la Usalama la Taifa, limesema.
Mtu
anayejitambulisha kama Luke Somers, ambaye alitekwa mwaka 2013,
ameonekana katika video, akisema maisha yake yako hatarini na anaomba
msaada.
Video hiyo pia inamwonyesha mfuasi wa al-Qaeda huko Yemen
akitishia kumuua Bwana Somers hadi madai yao ambayo hayajatajwa,
yatakapotimizwa.
Bwana Somers, mwenye umri wa miaka 33,
alifanyakazi kama mwandishi wa habari na mpiga picha wa mashirika ya
huko na kazi zake zikaonekana katika vyombo vya habari vya kimataifa,
ukiwemo mtandao wa BBC.
CHANZO. BBC SWAHILI.
Rais Robert Mugabe awalaumu baadhi ya wapinzani
wake ndani ya chama cha ZANU PF kwa kupanga kumuondoa mamlakani
Na JASMINE MUMWI.
Rais
wa Zimbabwe Robert Mugabe amelaumu baadhi ya watu ndani ya chama chake
tawala cha ZANU-PF kwamba wanapanga kumng'oa madarakani.
Akizungumza
katika kongamano la chama hicho, Mugabe amesema amebaini kuwepo
majaribio ya kuwahonga wajumbe kumpinga kama kiongozi, lakini
akasisitiza wajumbe hawawezi kupokea hongo.
Wanachama wengi wa chama hicho wangali ni wafuasi sugu wa Rais Mugabe
Mugabe ameahidi
kupambana na rushwa ndani ya chama na kukabiliana na maafisa wa chama
hicho ambao kazi yao ni kutoa hongo na kupokea rushwa.
Hasira ya Mugabe ilionekana
kufuatia madai ya njama ya kutaka kumuua yanayodaiwa kuandaliwa na
naibu wake Joyce Mujuru. Hata hivyo Mujuru alikanusha madai hayo ambayo
yamekuwa yakimuandamana.
Mugabe alisema kutokuwepo kwa Bi Mujuru kwenye mkutano huo wa chama kunaonyesha kuwa anaogopa.
Maelfu ya wajumbe wa chama walihudhuria kongamano hilo mjini Harare
Kadhalika Mugabe amesema Mujuru ni mwizi anayepanga kumuondoa mamlakani kwa kushirikiana na maafisa wengine wa chama. Chama tawala cha Zimbabwe
kinakumbwa na vita vya ndani kwa ndani kuhusiana na nani atarithi nafasi
ya Mugabe ambaye ana miaka 91 na ambaye ameongoza tangu uhuru wa taifa
hilo. Hata hivyo amekanusha madai ya kwamba anataka kujiuzuru na kusema kuwa huo ni upuuzi. Hivi
karibuni afisa mwingine mkuu wa chama tawala, Robert Gumbo aliiambia
BBC kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 90 amegeuza chama tawala na
kukifanya kama mali yake binafsi. Gumbo alisema lengo kuu la Mugabe ilikuwa kuendeleza uongozi wa chama kwa niaba ya mke wake Grace. Bi
Mujuru ambaye amekanusha madai hayo alionekana kama mtu ambaye
anechukua usukani wa chama kutoka kwa Mugabe ambaye walipigania naye
uhuru wa nchi hiyo kutoka mikononi mwa watwala wazungu. chanzo; BBC SWAHILI
Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imempa kiongozi wa mashtaka katika mahakama hiyo Fatou Bensouda muda wa wiki moja ili kutoa ushahidi dhidi ya rais wa Kenya, la sivyo aondoe mashtaka dhidi yake.
''Kucheleweshwa kwa kesi hiyo ya Rais Uhuru ni kinyume na maslahi ya haki.'' ilisema.Rais Kenyatta ni kiongozi wa kwanza wa taifa kufika katika mahakama hiyo tangu ashtakiwe rasmi mwaka 2012 na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu,ambayo ameyakana.Kiongozi huyo wa mashtaka ametaka kupewa muda zaidi ili kujenga kesi yake dhidi ya kiongozi huyo.Anasema kwamba mashahidi wamehongwa na kutishiwa maisha huku serikali ya Kenya ikikataa kutoa stakhabadhi muhimu za kesi hiyo.Bwana Kenyatta amekanusha kuchochea ghasia kufuatia mgogoro wa uchaguzi wa mwaka 2007 ili kumpatia ushindi aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki na kusema kuwa kesi hiyo ni ya kisiasa.
Akikataa ombi la kiongozi huyo wa mashtaka kuchelewesha kesi hiyo, majaji wa mahakama hiyo walisema kuwa wamempatia wiki moja Bensouda kusema iwapo ataitupilia mbali kesi hiyo ama ushahidi alio nao unaweza kuhimili kesi hiyo kuendelea.Rais Kenyatta alishinda uchaguzi wa urais mwaka 2013 kupitia usaidizi wa Mwai Kibaki.Aliitumia kesi hiyo kutafuta kuungwa mkono huku akiikashifu mahakama hiyo ya mjini Hague kwa kuingilia masuala ya Kenya.Ameshtakiwa na mahakama hiyo kwa kuhusika moja kwa moja katika mauaji ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008.Takriban watu 1,200 waliuawa katika ghasia hizo huku wengine 600,000 wakiachwa bila makazi.habari na JASMINE R MUMWI CHANZO BBC SWAHILI
Nahodha wa Manchester united Wayne Rooney, atafanyiwa uchunguzi zaidi ili kujua ukubwa wa tatizo la goti lake.
Rooney 29 aliukosa mchezo wa jana dhidi ya Stoke City uliomalizika kwa man united kupata ushindi wa 2 kwa 1, jeraha hili la goti alilipata katika dakika za mwisho za mchezo mwa ligi kuu ulofanyika jumamosi iliyopita kwenye mchezo na Hull City.
Meneja Louis van Gaal, amesema, "atafanyiwa uchunguzi zaidi na imani jeraha sio kubwa hivyo ila tunasubiri majibu ya uchunguzi”.
Bosi huyo wa man united anaamini Rooney na Di maria hawawezi kuwa fiti kuweza kuwakabili Southampton,
United imekua ikiandamwa na majeruhi wengi tangu kuanza kwa msimu huu ambako nyota wake kadhaa bado wako bechi kwa majeruhi.habari na veronica mramboah..bbc
Nchini Tanzania kuna maeneo machache ambayo baadhi ya watu wake hawana uelewa thabit wa kutumia mipira ya kiume(Condoms) kiasi ambacho mpira mmoja unaweza kutumiwa na vijana watatu hadi wanne kwa kubadilishana baada ya kuusafisha na kuanika juani.Hali hiyo imeelezwa kuwa chanzo kingine cha kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza alitembelea wilaya ya Longido kaskazini mwa Tanzania kijijini Orglay na kuzungumza na mmoja kati ya vijana wa kijiji hicho.HABARI NA VERONICA MRAMBOAH. BBC SWAHILI
Kama mwanzo wa makala ya hivi punde ya African Dream,mwanabiashara Mercy Kitomari-ambaye alianzisha kampuni ya kutengeza aiskrimu hai ya Nelwa's Gelato-anaeleza mbinu kumi bora anazotumia katika kuuza kwenye mitandao ya kijamii kwa wanabiashara chipukizi:
Anza na Lengo.
Kuna majibu matatu pekee yanayokubalika: a)kuongeza kujulikana kwa bidhaa zako kwa kufikia watu zaidi b)kujenga imani ya wateja kwa kuwapa usaidizi zaidi ama c)kuongeza mauzo kwa kutafuta wanunuzi zaidi,watakaonunua mara kwa kwa mara.Usianze kama huwezi jibu swali hili.
Wapuuze wapinzani wako- Kujaribu kuiba wateja wa watu wengine ni mbinu mbovu.Utaanza kuunda maamuzi mabaya kwa sababu unajaribu kuwafikia.
Fikra na kampeni bora zaidi bado hazijatendeka katika sekta yako.Angalia nafasi ambazo hazijaguzwa unazoweza kupata na kutumia.Tazama kile watu wanafanya kwenye sekta tofauti na ujaribu mbinu hizo.
Usiwe kwenye mitandao yote ya kijamii.
Usimamizi wa kijamii utamaliza rasilmali zako zote.Kila mtandao wa kijamii unaosimamia utakugharimu muda,pesa na nguvu zaidi,kwa hivyo amua zile utazipa kipao mbele.
Una pesa na wakati wa kutosha.
Watu huwa wanasema kuwa hawana muda na pesa za kuwekeza katika mitandao ya kijamii.Lakini ukweli wa mambo ni kuwa hauwezi kutowekeza.Kama hauna fedha za kutosha,inafaa uwe na wakati zaidi wa kuunda maudhui ama kuunda mtandao.
Mercy Kitomari ana mkahawa wa Nelwa's Gelato mjini Dar es Salaam inayosambaza kwenye hoteli na biashara zingine.
Weka lengo rahisi-
Kwa mfano,kuchapisha mara mbili zaidi kila wiki-ama kufikia bloga mmoja kwa siku.Pia fanya ukaguzi wa ndani kujua jinsi unavyotumia muda wako kwa sasa.
Mitandao ya kijamii ni bora,lakini watu wengi huchanganya kushikika na kazi na kuwa na ufanisi.Tambua shughuli zinazoleta ''mapato kutoka kwa uwekezaji'' ya juu zaidi,zipe kipao mbele na uweke mipaka.
Kuwa na nidhamu na kuwajibika kwa wengine.
Mwishowe,utahitajika kuchukua msimamo mgumu.Utahitaji kugawanya rasilmali zako chache na kuchagua kile utakachofanya (na kile utakachopuuza).Lakini utaona kuwa uamuzi huu ni rahisi kama una lengo.Matumizi yako ya mitandao ya kijamii yatakuwa na kusudi.Utapata kuwa una wakati wa kutosha wa kuitumia kimkakati.
Tambua kile kinachohamasisha wasikilizaji wako.
''Sekta'' ama ''biashara'' hazichoshi-watu wanaosema hayo ndio wanaochosha.Jinsi unavyojenga mawazo ya maudhui ya blogi ni kuelewa wasikilizaji wako na faida ambazo bidhaa na huduma zako zinawapa.
Mercy Kitomari anasema kuwa huduma ya wateja ni muhimu sana kwenye mitandao sawia na ya uso kwa uso.
Kuwa na sauti.
Watu hawapendi kuungana na mashirika yasiyokuwa na uso.Wanataka kuungana na wanadamu wa kweli.Hakuna atakayiependa,amini ama kuheshimu kampuni yako ikiwa hawezi kupata majibu yaliyo sawa na yenye uaminifu kwa wakati ufaao.Mitandao ya kijamii ni zaidi ya ''kujiingiza katika mazungumzo''.Ni njia mpya ya kufanya mambo,na vifaa kadhaa vipya kukusaidia kufanya hivo.
Lakini misingi ya njia za mauzo inabakia.Unahitaji kuvutia watu,kujenga imani yao na kuwawezeshakushiriki zaidi.
Tamba sana kupitia Facebook na Twitter.Mitandao ya kijamii namauzo kwenye mtandao inaanza na DNA yako,bidhaa ama huduma zako,na watu wako.Kwa hivyo kama unataka kuimarisha majibu yako kwenye mitandao ya kijamii,anda na kushughulikia utenda kazi wa ndani wa kampuni yako.Habari na VERONICAMRAMBOAH.chanzi bbc swahili