Mbunge wa Viti Maalum, Amina Abdullah Amour (CUF), ameitaka itunge sheria ya kuwataka viongozi wa umma kuorodhesha mali zao wanapostaafu ili kujua ni mali walizopata wakati wa uongozi wao.

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Nchi
, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya alisema kwa mujibu wa kifungu cha tisa (1) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya mwaka 1995, kiongozi wa umma anatakiwa kutoa tamko la rasilimali na madeni katika kipindi cha siku 30 baada ya kupewa wadhifa.
Alisema viongozi hao wa umma wanawajibika kufanya hivyo kila mwisho wa mwaka na mwisho wa kutumikia wadhifa wao.
Prof. Mwandosya alisema kwa kuzingatia matakwa ya kifungu hicho, upo utaratibu unaomtaka kiongozi wa umma kutoa tamko la rasilimali na madeni yake na kuliwasilisha kwa Kamishna wa Maadili anapostaafu au anapoacha kutumikia wadhifa wake.
Alisema kwa mujibu wa kifungu cha 15 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya mwaka 1995, kiongozi wa umma anayeshindwa kutoa tamko hilo kwa mujibu wa kifungu cha tisa au iwapo atatoa tamko la uongo au potofu katika kipengele chochote muhimu atahesabiwa amekiuka maadili.
Alisema kwa mujibu wa kifungu cha 27 (2) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya mwaka 1995, kiongozi yeyote wa umma anayetoa tamko la uongo kuhusu rasilimali zake, atakuwa ametenda kosa na atatiwa hatiani kwa kutozwa faini si chini ya Sh milioni moja na si zaidi ya Sh. milioni tano au kifungo kisichozidi mwaka mmoja.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment