NA ESTHER A CHAVALA.
12 Novemba 2014
Muuguzi
kutoka nchini Mali amekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola, kikiwa ni
kifo cha pili tangu Ugonjwa huo kudhibitishwa nchini humo.
Kesi hii haihusiani na ya kwanza ambayo msichana mwenye umri wa miaka miwili alikufa kutokana na Ebola mwezi oKtoba.
Shirika la Afya Duniani limetangaza mlipuko huu wa Ebola kama wa dharura duniani ambapo
Mtoto wa miaka miwili ndiye alikuwa wa kwanza kufariki kutokana na Ebola nchini Mali

Mtoto wa miaka miwili aliyefariki mwezi octoba.
Kesi hii ya Mali imeibuka siku moja baada ya shirika la Afya Duniani kuwatoa watu ishirini na tano karantini waliodhaniwa kumkribia msichana wa miaka miwili aliyefariki oktoba .
Miongoni mwa watu 100 waliokuwa karantini wameelezea kuwa kisa cha mtoto huyo kuugua na kufariki kutokana na Ebola kimewashangaza sana maafisa wakuu kwani inaarifiwa alisafiri kwa basi kutoka mjini Bamako kuelekea Guinea.
Takriban watu 5,000 wamefariki Afrika Magharibi kutokana na ugonjwa huo wa Ebola.
CHANZO CHA HABARI BBC SWAHILI.
0 comments:
Post a Comment