NA EMMA MOSHI
-
12 Novemba 2014
Kiongozi
wa kidini nchini Pakistani Abdul Aziz Ghazi anayemiliki shule nane zinazofundisha msimamo wa Bin Laden anatoa mafunzo ya fikra za Osama bin Laden
kwenye shule za dini kwa Wanafu
nzi takriban 5,000.
Ingawa serikali ya
nchi hiyo inapambana na wanamgambo wa Taliban kaskazini magharibi mwa
Pakistani, haina mipango ya kuzifungia shule hizo zinazotoa elimu kwa watoto
kuunga mkono wanamgambo wa Taliban.
Kiongozi huyo amesema wanatoa mafunzo kuhusu misingi ya Jihad ila ni juu ya wanafunzi kupata mafunzo ya kijeshi baada ya kutoka shuleni hapo.
Ghazi ambaye anamiliki shule nane za kidini yaani Madrasa,moja ya shule yake iliwahi kufanya ziara ya kwenda kukutana na Osama Bin Laden nchini Afghanistan.
Hivi sasa wasichana 3,000 na wavulana 2,000 wanasoma kwenye taasisi zake ambapo mitaala ya shule zake inatoa mafunzo ya kusoma Quran, kiarabu na thiolojia,hesabu na sanaa inaonekana kuwa masomo ya kidunia, vitabu vingi vimeandikwa na Ghazi na kuchapishwa katika shule hizo zenye vyumba vya kuchapisha.
Hata hivyo moja ya shule, zinazomilikiwa na Ghazi kuna maktaba iliyopewa heshima ya jina la bin Laden kutokana na ziara ya kwenda kumtembelea kiongozi huyonchini Afghanistan.
CHANZO CHA HABARI BBC SWAHILI
.
0 comments:
Post a Comment