NA GASPER MUSHI
Wanamgambo wa Dola la Kiislamu leo
wamechukua thuluthi moja ya eneo la mji muhimu wa mpakani nchini Syria, Kobane,
wakati Uturuki ikikataa kuyatuma majeshi yake kwenda kupambana na wapiganaji
hao wa jihadi.
Viongozi wa Jumuiya ya Kujihami ya
NATO na Marekani wanakutana leo na maafisa wa Uturuki ili kujadaliana kuhusu
mkakati wa kijeshi ili kusaidia kuwazuia wanamgambo hao
dhidi ya kuutwaa mji wa Kobani. Pande zote zinahofia kuwa mji huo unakaribia kuanguka mikononi mwa IS, lakini zinatofautiana kuhusu namna ya kuwasaidia wapiganaji wa Kikurdi wanaopambana ndani ya mji huo.
dhidi ya kuutwaa mji wa Kobani. Pande zote zinahofia kuwa mji huo unakaribia kuanguka mikononi mwa IS, lakini zinatofautiana kuhusu namna ya kuwasaidia wapiganaji wa Kikurdi wanaopambana ndani ya mji huo.
Mkutano huo wa siku mbili unaanza
leo mjini Ankara, ambapo maafisa wanatarajiwa kujadili kuhusu kitisho cha Dola
la Kiislamu kwa usalama wa Uturuki. Akizungumza baada ya mkutano na Katibu Mkuu
mpya wa NATO Jens Stoltenberg, Waziri wa Mambo ya Kigeni Mevlut Cavusoglu,
amesema Uturuki haiwezi kuchukua hatua kivyake.
Stoltenberg baadaye atazungumza na
rais wa Uturuki, waziri mkuu na waziri wa ulinzi. Marekani pia imewatuma
wajumbe kadhaa kushiriki katika mazungumzo hayo.
Marekani imefanya mashambulizi ya
kutokea angani katika maeneo ya IS, karibu na Kobane
Katikati ya mwezi Septemba, IS
ilianzisha mashambulizi katika mji wa Syria, Kobane, ambao uko karibu na mpaka
wa Uturuki. Wakurdi wamekuwa wakijaribu kuulinda mji huo, lakini hata wakati
Marekani ikiendelea kuyalipua na kuharibu maeneo ya IS, mapambano ya udhibiti
wa mji huo yanaonekana kuvunjika.
Rais wa Marekani Barack Obama
alijadiliana na makamanda wanaoongoza mashambulizi dhidi ya IS wakati jeshi la
Marekani likionya kuwa mashambulizi ya kutokea angani pekee hayawezi kulizuia
kundi hilo dhidi ya kuutwaa mji huo muhimu wa Syria. Akizungumza katika mkao
makuu ya ulinzi - Pentagon, Obama alisema haitakuwa rahisi kulishinda kundi la
IS lakini akasema kuwa muungano wa kimataifa unajitahidi kupambana na
wanamgambo hao wa Kisunni wenye msimamo mkali wanaoyateka maeneo ya Iraq na
Syria.
Uturuki imeweka vifaru vyake katika
eneo la mpaka karibu na mji wa Kobane, lakini hatua yoyote ya kijeshi
inayochukuliwa. Rais Recep Tayyip Erdogan ametoa wito kwa muungano wa kijeshi
unaoongozwa na Marekani kuyapeleka mjini humo majeshi ya ardhini. Akisema kuwa
kudondosha mabomu kutokea angani siyo suluhisho.
Erdogan kufikia sasa amekataa
kujiunga na operesheni hiyo inayoongozwa na Marekani bila kupewa ahadi na
Marekani kuwa pia itachukua hatua dhidi ya rais wa Syria Bashar al-Assad.
Wizara ya Ulinzi hata hivyo imeondoa uwezekano wa kuyapeleka majeshi ya ardhini
hasa baada ya operesheni za kijeshi zilizoshindwa kupambana na wanamgambo wenye
itikadi kali nchini Afghanistan na Iraq.
Wakati huo huo,waandamanaji wa
Kikurdi wanaokarishwa na hatua ya serikali ya Uturuki kushindwa kuchukua hatua
dhidi ya wapiganaji wa jihadi nchini Syria wamekabiliana na polisi kwa usiku wa
tatu mfululizo huku idadi ya vifo kutokana na vurugu hizo ikiongezeka hadi waru
22.
Huku wakikiuka amri ya kutotoka nje
iliyotangazwa na jeshi, mamia ya waandamanaji waliingia barabatani katika miji
ya Kikurdi kusini mashariki mwa Uturuki na wakatawanywa na polisi waliotumia
mabomu ya kutoa machozi na mizinga ya maji
CHANZO DW SWAHILI
0 comments:
Post a Comment