
NA; SINYATI KILUSU
Kampeni hiyo imeanzishwa chini ya
kaulimbiu ijulikanayo kwa lugha ya kiingereza kama ''I belong''. Shirika la
Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Wakimbizi-UNHCR limesema kupitia kampeni hiyo
linataka kuzimulika changamoto wanazokabiliana nazo watu wasio na uraia, na
kuzihimiza nchi kuzirekebisha sheria zao ili asiwepo mtu anayejikuta katika
hali ya kutokuwa raia wa nchi yoyote.
Mkurugenzi wa UNHCR Antonia Guterres
amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, kwamba kila dakika 10 anazaliwa
mtu asiyekuwa na uraia wa taifa lolote ulimwenguni, na kwamba kutokuwa na uraia
huwafanya watu hao kuhisi kama kuwepo kwao ni makosa. Guterres ameongeza kuwa
hilo halikubaliki katika karne ya 21.
''Watu wasio na uraia hunyimwa haki
zao za kimsingi, kama vile kuandikishwa kisheria wanapozaliwa, kwenda shule,
huduma za afya, ndoa na nafasi za ajira, na hata kunyimwa hati ya kifo pale
wanapoiaga dunia'', imesema ripoti ya shirika hilo.
Ukosefu wa uraia hutokana na sababu
nyingi
Watu wa jamii ya Rohingya: Myanmar
na Bangladesh zimekuwa zikiwatupiana kama mpira
Watu wanaweza kunyimwa uraia
kutokana na sababu mbali mbali, zikiwemo za ubaguzi wa kikabila, wa kimadhehebu
na hata wa kijinsia. Hali hiyo
pia
yaweza kutokea pale mataifa yanaposambaratishwa
na vita au mizozo.
Idadi kubwa ya watu wasio na uraia
hupatikana nchini Myanmar, ambako serikali ya nchi hiyo haiwatambui watu wa
jamii ya Rohingya ambao ni waislamu. Guterres amesema idadi ya watu hao ni
takribani milioni moja.
Myanmar huwachukulia watu hao kuwa
wahamiaji kutoka Bangladesh, nchi ambayo pia huwachukulia wale wanaovuka mpaka
kutoka Myanmar kuwa wahamiaji haramu.
Kusambaratika kwa mataifa
Idadi nyingine kubwa ya watu wasio
na uria wapatao 600,000 ilitokana na kuvunjika kwa Muungano wa Kisovieti wa
Urusi miaka zaidi ya 20 iliyopita.
Changamoto za kukosa uria pia huwakumba watu
waliozikimbia nchi zao. Kwa mfano, asilimia 70 ya watoto wanaozaliwa na
wakimbizi kutoka Syria walioko Lebanon na Jordan hawapati vyeti vya kuzaliwa, amesema
Antonio Guterreschanzo DW SWAHILI
0 comments:
Post a Comment