Habari na; KEPHAS DANIEL
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetangaza kuwa, migogoro ya Syria na Iraq imesababisha kuwepo wakimbizi milioni 13.6 na kuleta hali mbaya ya kibinadamu katika baadhi ya maeneo ya nchi hizo.
Ripoti ya shirika hilo imeeleza kuwa, wengi wa wakimbizi hao wanaishi bila chakula na makazi huku msimu wa baridi ukianza.
Idadi hiyo inajumuisha watu milioni 7.3 ambao ni wakimbizi ndani ya Syria, milioni 3.3 walioomba hifadhi nje ya nchi, milioni 1.9 wakimbizi ndani ya Iraq na laki na 90 elfu ambao wako katika nchi jirani.
Amin Awadh Mkurugenzi wa UNHCR Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika amesema kuwa, wakimbizi wa Syria wamekimbilia katika nchi za Lebanon, Jordan, Iraq na Uturuki na kuzitaka nchi nyinginezo hasa za Ulaya kufungua milango ya mipaka yao ili kuwapokea wakimbizi hao.
Ameongeza kuwa, Russia na China zinaongoza kwa kutoa misaada kwa ajili ya wakimbizi wa Syria.
Chanzo; Tehran Swahili

0 comments:
Post a Comment